Procedure zikoje katika kumiliki ardhi kuanzia watu wawili kwa pamoja hapa Tanzania?

Wadau naomba kujua hizo taratibu moja baada ya nyingine.
Sheria inaruhusu umiliki wa ardhi wa pamoja ya joint tenancy au tenancy in common.

Procedure hazitofautiani na zile individual ownership isipokuwa certificate of title itakuwa inaonyesha hiyo ardhi inamilikiwa kwa joint tenancy au tenancy in common.

Naona uzi umetelekezwa.
 
Taratibu ziko kawaida, watu hao wanamilikishwa kwa hati ya pamoja.

Ikiwa wamiliki ni mme na mke, wanaweza kumilikishwa kwa joint occupancy. Katika aina hii ya miliki, akifa mwenza, moja kwa moja aliyebaki anamiliki hati peke yake bila kujali kama aliyefariki ana warithi wengine.

Hii joint occupancy hairuhusiwi kwa watu ambao sio mke na mme, vinginevyo ikihitajika lazima kupata kibali cha mahakama.

Aina ya pili ambayo watu zaidi ya mmoja wanaweza kumiliki ardhi ni occupiers in common. Yaani kila mmoja anakuwa na hisa zilizoainishwa. Yaweza kuwa occupiers in common in equal shares yaani hisa sawa au zaweza kutofautishwa mfano watu wawili 1/3 na 2/3 share au mfano wa wamiliki watatu 10%, 30% na 60% share nk.

Occupiers in common ndiyo hasa hutumika kwa umiliki wa pamoja wa watu wasio wanandoa. Mmoja akifa, hisa zake zinaenda kwa warithi.
 
Back
Top Bottom