Probability ya kuoa na kuolewa

Probability ya kuoa na kuolewa

hizi ndo mada za kijinga jinga ambazo zinatrend jf siku hizi

ukitoa mada ya maana mada inafutwa au unaishia kupigwa ban kwa kuwa umemchambua mtu wa kwenye system.

jf na fb siku hizi hakuna tofauti.

jf ushilawadu tuu
utakula ban sasa hivi!
 
Kuolewa ni bahati, kuoa ni kuamua!
 
huu utafiti wako ulikua sponsored na taasisi gan?
 
Baada ya kufanya utafiti
na kuridhika nao. Sasa tumeamua kuutoa mbele ya watanzania! Kama hujui hesabu hasa Probability sasa iko hivi, probability ni uwezekano wa kitu fulani kutokea sasa leo tunaenda kuzungumzia uwezekano wa mtu kuolewa au kuoa:

WANAWAKE

1. Ukiwa una tabia nzuri ila shape na sura haujafinikiwa uwezekano wa kuolewa ni asilimia 40%

2. Ukiwa una tabia nzuri shape nzuri ila sura haukufanikiwa uwezekano wa kuolewa ni asilimia 70%.

3.Ukiwa na sura nzuri shape nzuri na tabia nzuri uwezekano wa kuolewa ni asilimia 85% kama hauna mtoto. Na kama una mtoto ila haukai naye ni asilimia 65%

4. Kama umezaa mtoto na uko unaishi naye yaani hana pa kwenda basi uwezekano wa wewe kuolewa na mtu ambaye sie baba wa mtoto ni 30% .

5. Ikijulikana wewe ni kicheche mtaani kwenu haujatulia basi uwezekano wa kuolewa ni asilimia 5%. Ila uwezekano wa kupewa mimba na kuachwa ni asilimia 80%.

6. Ikijulikana wewe ni bikra mbele ya watu na wakajua wakawa na uhakika basi uwezekano wa kuolewa ni asilimia 93.5%.

Kwa wanawake ikumbukwe kila degree unayoongeza kwenye kusoma inapunguza uwezekano wa kuolewa sasa basi:

7. Kama una degree moja uwezekano wa kuolewa ni asilimia 70%

8. Kama una masters basi uwezekano wa kuolewa ni asilimia 45%.

9. Kama una PHD basi uwezekano wa kuolewa ni asilimia 15%

10. Kama umekuwa Profesa basi dada yangu uwezekano wa wewe kuolewa ni asilimia 2%.

11. Kama una matege na ndo changamoto yako basi dada ukivaa sketi siku zote uwezekano wa kuolewa unakuwa asilimia 70%. Lakini kama unavaa suruali kuonyesha matege yako miguu inazunguka zunguka kama feni basi uwezekano wa kuolewa ni asilimia 3%. Na hawa wanaume watakaokuoa ni wale vipofu!

12. Kama umezalishwa watoto kama watatu na hujaolewa basi wewe uwezekano wa kuolewa ni asilimia 2%.

13. Kama unashinda online kazi kupost picha insta, whatsapp, facebook, panyabuku na countabuku basi uwezekano wa wewe kuolewa ni asilimia 15%.Yaani kila mwanamume anahisi wewe ni mali ya uma.

14. Kama wewe ni kibonge sana basi uwezekano wa kuoelewa ni asilimia 50%. Punguza kula dada yangu. Ukishaolewa kula nenepa mpaka upasuke.

15.Kama wewe ni mwembamba sana basi uwezekano wa kuolewa ni asilimia 40. Nenepa kidogo!

16. Kama unatumia simu ya TECNO uwezekano wa kuolewa ni asilimia 70%.

17. Kama unatumia Iphone basi uwezekano wa kuolewa ni asilimia 10%.

18. Kama una marafiki wengi wa kiume kuliko wa kike. Basi uwezekano wa kuolewa ni asilimia 30%. Utasema hao ni marafiki ila kumbuka wanaume hawaaminianagi. Wewe pia utaonekana ni mali ya uma hata kama sio!

19. Kama unanuka mdomo. Dagaa sijui wa juzi ulikula basi uwezekano wa kuolewa na wewe ni asilimia 20%. Hamna mwanamume ambaye yuko radhi atapike siku akiambiwa "You can now kiss the bride!"

Naona mpaka hapo mtakuwa mmeelewa maana ya probability na mnaweza kucalculate za kwenu. Haya tuamie kwa jinsia zilizobaki

WANAUME
1. Kama hauna hela uwezekano wa kuoa wewe ni asilimia 0%
Xe.
2. Kama una hela basi uwezekano wa wewe kuoa basi ni asilimia
100000% au unaweza hata ukaoa kijiji kizima.

Simple sana kwa mwanaume‍♀‍♀‍♀
Kwa wanaume, kuwa na hela, kuowa siyo probability tenaaa... NI SURE EVENT
 
Mbona total % zinavuka 100
Huwa hawajumlishi probability ya vitu viwili kila kimoja kinajitegemea mkuu, ngoja nikusaidie hapo ni kujumlisha probability ya kuolewa na kutokuolewa katika kila point
 
Back
Top Bottom