Wadau kama utamaduni wetu wa Kitanzania nimewekewa pressure ya juu sana ya kuoa!. Umri wa miaka 38 kwenda 39 sasa pressure imekuwa juu sana kama unavyojua utamaduni wetu. Mimi nilivyokuja US kama vijana wengi ambao tulimaliza shule miaka ya kati ya 1990's tulikuwa hatujui vizuri tunakuja huku kwenye nchi nyingine na mazingira yatakuwaje. Hivyo vijana wengi tumeanza kuwa wenyewe bina watu wazima wa kutuangalia au kutupa mawazo kuanzia miaka 21!. Pamoja na kuwa na uhuru wa hali ya juu hasa hapa USA vilevile tumekuja kwenye utamaduni wa kujitegemea sana. Mapema sana kwenye safari yetu ya maisha ya hapa ilibidi tuchague maisha gani tunataka kuna waliochagua kujirusha, kupiga deals na kujichanganya na wengine tuliamua kujaribu kujisomesha na kutafuta kazi au biashara huko mbele.
This is deep and very relatable. Mimi nilienda kupiga boksi nikiwa bado teenager. Kwa hiyo kimsingi nimeanza kuishi peke yangu mbali na wazazi wangu nikiwa na umri mdogo sana.
Kwa watu ambao hawanijui, wanaweza kudhani labda nimekulia kwenye mazingira fulani ya kudekezwa hivi. La hasha! Maisha ya Marekani kama huna skills za maisha ni magumu sana hususan ukiwa bado mdogo.
Nisingekuwa na nidhamu, hekima, busara, na common sense basi leo hii ningekuwa nimeshafulia kabisa na huenda hata ningekuwa jela au marehemu.
Lakini nashukuru kubahatika kurithi sifa bainishi ya common sense kutoka kwa mmoja wa wazazi wangu (nadhani kama siyo mama mzazi basi atakuwa babu mzaa mama).
Peer pressure ni kitu kibaya sana. Nimeona jamaa wengi sana waliokuwa wanabeba boksi waliopotoshwa na hizo pressure na sasa maisha yao hayana mbele wala nyuma.
Tatizo lingine ni kwamba unavyozidi kuwa mtu mzima vitu viwili vinajitokeza kuhusu mahusiano (1) Unakutana na wanawake wengi wenye matatizo sana kwenye background zao (2) Unakuwa na akili sana ya kiutu uzima na unajua weakness haraka sana za watu. Kuwa smart sana kwenye mapenzi wakati mwingine sio nzuri. Napenda kuwa na familia lakini sitaki kuwa tu na mtu yeyote kwa sababu ya kuwa na familia.
Hii observation nayo iko on point sana hususan hiyo namba mbili. Kwa watu analytical na observant kama mimi, hii sifa ni baraka na laana.
Binafsi huwa nachanganua hadi cadence ya mtu. Na kwenye observation huwa naenda mbali mno hadi najistukia mwenyewe.
Hivi kwa mfano tu, ni nani humu huwa anajaribu kuangalia kama mwanamke ana nose hair zilizochomoza? Na kama anazo kwangu ni kama deal breaker flani hivi.
Kwa hiyo nakuelewa kabisa unaposema wakati mwingine ukitumia akili (na ukiwa na akili sana) kwenye mapenzi si vizuri kabisa. Kila utayekutana naye utamwona ana kasoro tu na labda hakidhi vigezo vyako na blahze blahze kama hizo.