Press ya Mnyika yawavuruga CCM

Nimesikitika kuona hata TBC nao wanahusika na hizi propaganda. Hii Hali ina athari kubwa Sana kwa utendaji wa mkuu wa nchi. Bado miaka mitatu kufikia kipindi Cha kuanza propaganda za uchaguzi ila ukianza Leo maana yake lazima uache kuwatumikia wananchi uwatumikie viongozi wa CcM na watoto wao. Si muda wakuangaika kutumia pesa za walipa kodi kulipa watu wafanye propaganda ni muda wakutenganisha urais na shughuli za chama.

Naomba nitabiri na kama Rais akitumia utabiri wangu atakubaliana na Mimi " Ikulu, kwenye chama na ndani ya vyombo vya dola wapo watu wanatajirika kupitia mradi huu wakupambana na upinzani. Watu Hawa wanatumia mwanya huu kupokea fedha serikalini kusafiri nchi nzima kwa mambo yasiyokuwepo na ambayo hayawezi kufanyiwa auditing. Naamini kwa uzoefu wangu kwenye ualimu wapo watu kutoka makao make ya wizara,idara na state wanatengeneza propaganda mikoani then wanajilipa kwenda kuzitatua tuweni makini nao. Naamini hata kwenye dola wanaojenga maghorofa ni wale walioofisi nyeti ya nchi ambao kwa kipindi Cha mwalimu walikuwa hawaruhusiwi kuzikumbatia fedha haramu, wanaotisha watu bar ni watu wa ofisi nyeti, wanaotisha watu wauziwe ardhi ni watu wa ofisi nyeti, wanaofanya anasa ni watu wa nyumba nyeti na si kutoka ofisi zote Bali kutoka makao Dodoma na Dar. Hawa watu wanatoa wapi fedha kipindi hiki? Wanasafiri huko mikoani hakuna watu wakufanya hizo kazi? Hawa ndio wanaelekeza watu wasitolewe mahabusu Hadi wafike wao, Hawa ndio wanaowaelekeza ma RPC wafanye nn? Tusipowadhibiti tukaona wananufaika ipo siku waliopo mikoani watagawanyika kutaka kwenda huko juu kwa kuchoshwa na maelekezo ya watu wapumbavu.

Nchi haina Tena nidhamu, wasimamizi wa nidhamu wamekuwa watovu na nidhamu. Kijana wa Tiss ana few years kazini anapata wapi fedha zakujenga ghorofa? Anapata wapi jeuri yakutisha watu bar kwamba atawafix? Ipo siku wakiendelea kuzoea kupata madili machafu siku wakiyakosa watakuwa waasi, turudishe nidhamu ya jeshi, idara nyeti na taasisi nyingi, tuwajengee uwezo lakini TUKIRUHUSU CONSTABLE WA MAKAO MAKUU AKAWA NA NGUVU KULIKO OCD TUTAVUNA TUNACHOPANDA ALIYASEMA MWALIMU WETU WA JKT MIAKA YA TISINI KWAMBA UKUBWA WA ASKARI SIYO KITUO NI MABEGA.
Bado tu hawajajifunza faulo za magufuli? Kweli Kenge hasikii......
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom