Press kuhoji utolewaji wa ajira mpya. 15-10-2016.

Press kuhoji utolewaji wa ajira mpya. 15-10-2016.

Press Conference kuhoji ni lini ajira mpya zitatoka itafanyika leo tarehe 15 saa sita kamili Mchana, Mahali ni Mwananyamala hospital.

Pesa kamili iliyopatikana ni shilingi 124,000/= na Kuna Miamala mimili tu mipya, hivyo hatujafikia lengo la bajeti.

Tutume kwa wingi michango na wakaofika wabebe (500 au 1000) kuongezea mchango kwaajili ya kulipia media.

Wahanga na wadau wote Inatakiwa kuwahi saa moja asubuhi kuangalia uwezekano wa kuongeza vyombo vya habari na kuandaa eneo husika.

kwa mawasiliano piga 0717389255

Peleka pesa uliwe.Kikao mwananyamala hospitali!!! Watu wa kutapeliwa wanatafutwa hapo.Abiria chunga mzigo wako wa hela
 
Ujinga kwako, maarifa kwa wengine.
Ni kweli,mimi pia ni mhanga wa ajira na hawa ni wenzangu ila SIWEZI KUUNGA MKONO VIJANA WANAFKI,WACHUMIA TUMBO,maslahi yao yakiguswa midomo juu,nchi inaharibiwa maslahi ya vizazi na vizazi yanaharibiwa wapo kimya,mpaka waguswe wenyewe,WANAFKI WAKUBWA.
 
Hal imekuwa mbaya vijana wanataabika jua lao mvua yao wakitafuta maisha lakn hakuna unafuu wowote. kwa hal kama hii ikiendelea social evils lazma ziongezeke ili watu wapate kujikim kimaisha
 
FISIEM kiboko aise. Halafu inajitapa inawajali maskini?
Hawa jamaa siyo wa kuamini kbsa hata hizo sera zao za viwanda tumepigwa changa la macho
Uhakiki tu umewatoa jasho mwaka sasa,viwanda watawezea wapi?
 
Ujinga upi?
Ajira za maskini mnataka mzifanyie mtaji wenu?
Hamjaridhika na mafao ya wanyonge bado na ajira zao mnataka mzifanye km sehemu ya kujiongezea utajiri na familia zenu.
Nyie wabaya sana. Mnataka mhakikishe maskini hana kitu km ndiyo mridhike.
Kweli FISIEM NI FISIEM TU
Nitake radhi mzee,sijawahi kuwa CCM na sita kuwa milele,LAKINI SIWEZI KUBALI KUUNGANA NA VIJANA WANAFKI,Vijana wasiojua maslahi ya wengi zaidi ya yao,ushawahi sikia wapi vijana hawa wanaongea nchi inapokwenda mrama,umewahi sikia wapi wanaongea dawa zinapokosekana hospitali,wapi uliona wanaongea katiba inavyovuliwa nguo? Matumbo yetu yameguswa ndo tunajifanya tunauchungu,HAPANA BOSS.
 
NASISI SECTOR ZA KILIMO NA SOCIOLOGIA AMABAO TULIKUWA HATUAJILI ZAMANI TUNASITAHILI KUIRADHIMISHA SERIKALI KUTUPA KAZI?
Sijui kwa upande wenu. Ila Hii ni ya walimu, watu wa afya, polisi na Jwtz
 
Press Conference kuhoji ni lini ajira mpya zitatoka itafanyika leo tarehe 15 saa sita kamili Mchana, Mahali ni Mwananyamala hospital.

Pesa kamili iliyopatikana ni shilingi 124,000/= na Kuna Miamala mimili tu mipya, hivyo hatujafikia lengo la bajeti.

Tutume kwa wingi michango na wakaofika wabebe (500 au 1000) kuongezea mchango kwaajili ya kulipia media.

Wahanga na wadau wote Inatakiwa kuwahi saa moja asubuhi kuangalia uwezekano wa kuongeza vyombo vya habari na kuandaa eneo husika.

kwa mawasiliano piga 0717389255
Hivi Ajira zinatolewa kama biskuti??? Kama ajira zinatokana na wingi wa kazi viz avis wafanyakazi, Maoni yangu ni kwamba kwenye sekta ya umma kuna wafanyakazi wengi zaidi wanaohitajika na vilevile kuna misallocation of manpower.
Ili kuleta ufanisi ninadhani kwa sasa ingefanyika manpower audit ili kufahamu mahitaji halisi na watakao zidi wapewe nafasi ya kuondoka hivyo hoja ya kutoa ajira ya ziada haipo [ila kwenye seckta nyeti kama madaktari/nurses etc.
 
Kama mtu hatatiwa korokoroni kwa kuchangisha fedha bila kibali, na kuitisha mkutano pasipo kibali ... Stay tune!
 
Subiri mamlaka husika baada ya safisha safisha ya watumishi hewa na uhakiki
 
Press Conference kuhoji ni lini ajira mpya zitatoka itafanyika leo tarehe 15 saa sita kamili Mchana, Mahali ni Mwananyamala hospital.

Pesa kamili iliyopatikana ni shilingi 124,000/= na Kuna Miamala mimili tu mipya, hivyo hatujafikia lengo la bajeti.

Tutume kwa wingi michango na wakaofika wabebe (500 au 1000) kuongezea mchango kwaajili ya kulipia media.

Wahanga na wadau wote Inatakiwa kuwahi saa moja asubuhi kuangalia uwezekano wa kuongeza vyombo vya habari na kuandaa eneo husika.

kwa mawasiliano piga 0717389255
wajinga ndio waliwao
 
Habari wadau,
Tunashukuru Mungu mkutano wetu vijana wahanga wa Ajira na Wandishi wa Habari umefanyika japo tulipata changamoto ya kukamatwa na Polisi wa Wilaya ya Kinondoni na kisha kupelekwa Kituo cha Polisi Oysterbay.

Baada ya mahojiano kwa muda wa masaa kadhaa hatukupatikana na HATIA na kisha kuruhusiwa kuendelea na Press Conference ambapo Waandishi kadhaa wa baadhi ya vyombo vya habari nao waliingia katika kadhia hiyo kisha badae kuachiwa huru.

Kwa kipekee namshukuru Mkuu wa Polisi Wilaya ya Kinondoni (OCD) LISSU NTANDUU kwa kutuachia na kuruhusu kuendelea na mkutano na Waandishi wa habari lakini pia kwa kufanya kazi kwa Weledi mkubwa, hakika ni mfano wa kuigwa kwa polisi wengine.

Hivyo taarifa yetu ya Kumuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dr. John Pombe Joseph Magufuli atoe Tamko Rasmi zitatoka katika vyombo vya habari zikiwemo Televisheni, Radio na Magazeti kuanzia kesho.

Namshukuru pia OCD Kinondoni kwa kuisoma taarifa yetu vyema sana na kuikubali kwa asilimia zote huku akipongeza ustadi mkubwa tulioutumia katika kuandika Taarifa hiyo na kusema kweli ni ya Kisomi kabisa.

Mungu akipenda taarifa hiyo nitaipost hapa kesho kama mtapenda kuisoma pia.

Asanteni kwa Umoja wenu.
 
Back
Top Bottom