President Zuma Advises Museveni to Rename Lake Victoria

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Feb 17, 2016
17,506
15,999
Rais Zuma ataka Ziwa Victoria libadilishwe jina

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa eneo hilo.

Rais wa Afrika Kusini, Jacob Zuma ameitaka Uganda kubadili jina la Ziwa Victoria ili liendane na jina linalowakilisha uhalisia wa wananchi wa eneo hilo.

Kiongozi huyo anayekosolewa vikali nchini mwake amesema tayari amemfahamisha Rais Yoweri Museveni juu ya haja ya kubadilishwa jina hilo.

Jina la Ziwa Victoria lilitolewa na mtafiti mmoja wa Uingereza kama zawadi kwa Malkia wa Taifa hilo aliyetambulika kwa jina la Victoria.

Akizungumza katika ufunguzi wa maonyesho ya utalii mjini Kampala, Rais Zuma amesema Ziwa hilo kuendelea kuitwa Victoria kunawanyima fursa wananchi wa eneo hilo kujivunia uasili wao.

“Mnaweza kuweka bango kubwa linaloonyesha jina la jipya na kisha mkaweka bango dogo litakalosomeka kama “ zamani eneo hili liliitwa Ziwa Victoria”. Lazima mbadilishe jina hili na kuweka jina litakaloelezea uzuri wa Taifa hili,” amesema Rais Zuma.

Rais wa Afrika ya Kusini Mh. Jaco Zuma amependekeza kubadilishwa jina la ziwa Victoria na kuitwa jina la kizalendo.

Jina la ziwa Victoria lilitoloewa na mwandishi mmoja wa habari wa Kiingereza aliyetoa jina hilo kama zawadi katika siku ya kuzaliwa Malkia Victoria wa Uingereza.

Kadai kuwa ashamtwangia uzi hata rais wa Uganda naye aunge mkono hoja hiyo ya kubadilishaq jina la ziwa hilo kubwa kuliko yote Afrika.

Nini maoni yako mkuu juu ya pendekezo hili la mkuu Zuma.?
 
Uganda ibadilishe jina la ziwa ambalo liko kwetu zaidi ya nusu? Mmh! Ndo maana wanakuzodoa sana hukp kwenu!

Nadhani Zuma kwa elimu yake ya Grede 4 anajua ndivyo inavyokuwa kwa maziwa yaliyo shared kati ya nchi - kama alivyoona Malawi ziwa wanaliita Lake Malawi kwao na kwetu ni Lake Nyasa. Sijui Msumbiji wanaliitaje, Nyasa au Malawi?
 
Hizi ndio akili za waafrika. Kubadilisha majina ya kizungu huku wao binafsi ni mafisadi wa kutosha. Hata Mobutu alikataa jina lake la kwanza akajiita kuku
 
hii kitu ilikuwa inaniumiza sana kichwa, na nikiwa primary niliwahi muuliza mwalimu wangu kwanini lisiitwe jina la kwetu badala ya kuitwa victoria, huyu victoria ni nani, kwa kweli alinipa jibu ambalo sikuridhika nalo, sasa viongozi wetu hata 1 hakuwahi kuwa na wazo hili, leo hii zuma kaamua kusema, hata mie naungana nae, wacha tuone, mara asiyepangiwa anaweza akagoma kwai hapangiwi
 
Rais wa Afrika ya Kusini Mh. Jaco Zuma amependekeza kubadilishwa jina la ziwa Victoria na kuitwa jina la kizalendo.

Jina la ziwa Victoria lilitoloewa na mwandishi mmoja wa habari wa Kiingereza aliyetoa jina hilo kama zawadi katika siku ya kuzaliwa Malkia Victoria wa Uingereza.

Kadai kuwa ashamtwangia uzi hata rais wa Uganda naye aunge mkono hoja hiyo ya kubadilishaq jina la ziwa hilo kubwa kuliko yote Afrika.

Nini maoni yako mkuu juu ya pendekezo hili la mkuu Zuma.?
Angetuambia anataka liitweje,,
 
Back
Top Bottom