President Speech and His Personality | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

President Speech and His Personality

Discussion in 'Great Thinkers' started by Profesa, Aug 1, 2012.

 1. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #1
  Aug 1, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  Niliwahi kusema hapa kwamba wanaomshauri raisi na kumuandikia Hotuba walikuwa wanaboa, kwakuwa hawakuwa hata wana-capture issues muhimu na kumfanya Raisi aongelee vuvumi na mambo ambayo mengine hayakupaswa kuzungumziwa na nafasi ya Uraisi. Niliongelea pia jinsi raisi anavyopresent ilivyokuwa inaboa.

  Lets be realistic, tuache ushabiki wa kijinga, no matter how bad we felt about our president, binafsi niko so impressed na setup ya hotuba ya leo (Ya Mwisho wa Mwezi wa July 2012), from the audience aliyoihutubia mpaka jinsi alivyokuwa anazungumza. Ni tofauti na wakati mwingine maana kuna wakati nilifeel ni puppet inaongea it was o boring yeye kuongea na screen na si kuongea na watu. Well done Washauri wa kipindi hiki na well done president for thinking out of the Box. You have skipped so many unnecessary critiques. I even enjoyed the way you present your issues, in a very presentable meeting the language and expression of many. Nimefurahi sana jinsi ulivyokuwa unachambua ishu umeonekana hujakariri unajua unachoongea hasa na unavutia kama Raisi. Nawachukia waliokuwa wanakupotosha.

  Hapa anaonyesha yeye siyo Raisi wa CCM kuongea na Wazee wa CCM ambao mda mwingi wanasinzia anapokuwa wanahutubia hotuba yake ya Masaa 3, na kuongea na Screen akiwa ameganda utadhani amekariri akiwa anateswa na taa za studio huku wakati mwingine machozi yakitaka kumtoka, ukizingatia na suti hadi jasho linakuwa linamtoka.

  Hon President never go back to that situation.
   
 2. M

  Mkandara Verified User

  #2
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Profesa Hotuba hiyo iko wapi?..
   
 3. Profesa

  Profesa JF-Expert Member

  #3
  Aug 2, 2012
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 902
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 45
  LInganisha hapa: Rais Jakaya Kikwete na hotuba ya kila mwisho wa mwezi - YouTube na MICHUZI: HOTUBA YA MHE. DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE, RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, KWA WANANCHI, TAREHE 1 AGOSTI, 2012 bado sijapata video ningeweza kuweka hapa, ili kulinganisha PR na jinsi anavyo manage audience na madudu waliokuwa wakimshauri kuyafanya wakati wa hotuba za Mwezi ila hotuba kamili hii hapa: https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/301419-rais-kikwete-akutana-na-wahariri%3B-asema-madai-ya-walimu-hayatekelezeki.html Nadhani inabidi awe natural and realistic awe the real Kikwete sio actor au imitator of the imaginary scene Wa- Tanzania wanakaribia kukata tamaa. Akizungumza hivi angalau mara kwa mara kutemeana na substancial issue then we will be moving, asijichimbie Riasi uko juu please make use of the remaining time you can leave behind a memorable history you still have a chance to do that, usiridhike bado wananchi hawaelewi hata kama wewe unadhani umefanya makubwa unapaswa kuendlea kutafuta means za kuwaelewesha na kuwatia moyo. Maadui wako utawashinda kwa kuwa real Kikwete just as you did this time. Never talk to CCM people on significant national issues, you are the president of all people regadless of their political, faith, cultural, social or economical position. remember that.
   
 4. M

  Mkandara Verified User

  #4
  Aug 2, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  @Profesa, binafsi yangu usanii huu hata siku moja hauwezi kunivutia....Waswahili tunasema anayelia sana msibani huwa ndio mchawi..Binafsi sikuridhika na hotuba hiyo kwa sababu ni acting nzuri sana kushinda Oscar ya sinema, kitendo cha kuonyesha mtu akilia ndani ya suti kali na ya gharama..Hotuba haiko realistic ni mazingaombwe tu.. Kilichofanyika hapa ni reaction as to disaster recovery! hakuna zaidi ya kilio cha mchawi kurudisha imani za watu kwamba sii yeye mchawi bali kazi ya Mungu..Kama serikali ingekuwa imejiandaa vya kutoisha na swala hili limetokea tungesema well sababu ni hii lakini hizi sababu zimeanza toka Meli ya MV Bukoba na zinaendelea hadi kesho..

  Ukitazama ajali ya Meli zilizotokea Zanzibar haiwezi kuwa ndio Uamasho kwetu ya kufikia makubaliano ya sheria na taratibu wakati hata Bara Meli zilisha zama na wala sii moja. Hivyo tunapokubaliana kuwa na sheria moja ina maana gani kusaidia ajali ikiwa hata bara sheria zipo isipookuwa zinakiukwa siku baada ya siku na kila inapotokea ajali tunamsingizia Mungu..The fact ni kwamba tumeshindwa kabisa kuondoa UHABA wa vitu nchini toka majumbani, ajira, maisha, shule, Hospital, Usafiri na hata nguo nadio maana tunavaa mitumba zaidi.. Na maadam kila ktu tunategemea kuagiza nje Uhaba huu hautakwisha na hizo sheria zitabakia vitabuni kwa sababu hakuna nchi inayoweza kutumia sheria palipo na UHABA (Scarsity)..Uhaba ndio chanzo cha Corruption na kama hakuna vita ya corruption, sheria haiwezi kuwapa kinga wananchi..

  Ebu tazama ajali za barabarani.. umewahi kumsikia rais akizungumzia? Je unajua ya kwamba mwaka jana tu wamekuwa zaidi ya watu 20,000 na mwaka uliopita.. tuseme ktk miaka sita iliyopita wamekufa watu zaidi ya 100,000 kwa ajali za barabarani tu..Tumeshindwa kutazama ubora wa Daladala, Mabus, Malorry, Meli, reli yaani kote huko yanaua watu kila siku, tumeshindwa kusimamisha sheria kwa vitu tunavyokutana navyo kila siku barabarani itakuwa meli baharini?..itawezekana vipi swala la meli naa usafiri wa majini wakati tuna shida kubwa ya vyombo hivi vya usafiri.. Watu wataendelea kubeba abiria zaidi ya idadi na tutaendelea kutumia sheria mbovu kwa sababu tumeshindwa kukidhi Uhaba uliopo.

  Swala ma Mafuta na gas:-
  Watanzania hawataki kujua habari za visima vingapi vinachimbwa bali rais anawahakikishia wananchi ni kiasi gani cha asilimia serikali yetu inamiliki au itamiliki ktk visima vilivyokwisha patikana na kutoa gas. Na binafsi yangu hadi kesho sintokubaliana na wazo la kuvuta gas Dar ati kwa sababu ya ahadi ya kuzalisha megawatts 3,500 ambaoz zinategemewa kupatikana kufikia mwaka 2015..Huu ni usanii mwingine kabisa na kwanza hizo 3,500 ni total megawatts tunazozitegemea kutoka uzalishaji wa aina zote sio gas tu.. Hizi sasa tuna megawatts 350 ktk gridi ya taifa hizi zote ni za dharura ambazo hatuwezi kujivunia.. Sasa tunapeleka Bomba Dar ili kulishwa vyombo gani?.. Tanesco wameisha agiza mitambo ya kuzalisha umeme ya mega watts ngapi hadi tulete bomba la gas Dar?..Halafu huwezi kutumia gas sehemu moja maana kusafirisha umeme ndo ghali zaidi. Kwa nini wasianze na kuzalisha Umeme huko huko Mtwara, Lindi na Pwani na kama kunatalkiwa bomba la kuja Dar basi litoke Pwani kwa sababu ni karibu na litaweza kuzalisha umeme kwa ajili ya Dar..

  Kama kweli tunataka kuzalisha Umeme wa gas Dar basi hii haitakuwa na maana yoyote kwa mikoa ya Mbeya Sumbawanga, Iringa hadi Kigoma na Tabora kwa sababu tutaendelea kusafirisha Umeme na sio gas kutoka Dar kwenda maeneo hayo kwa kupitia gridi ya Taifa. Hatuta save cost zozote. Kinachotakiwa kufanywa ni kuweka mipango sawa, wazi na cheap kwa watumiaji.

  Matumizi gas majumba ya watu:-
  Ni kweli Gas ilitumiwa sana na nchi za magharibi ktk mageuzi ya kiuchumi toka miaka ya 30 hadi 60 lakini miji mingi hawatumii tena gas majumbani kutokana na hatari zake, hivyo nyumba nyingi za kisasa wanatumia majiko ya Umeme badala ya gas kwenda moja kwa moja majumbani. Kweli gas ni rahisi Cheap lakini p[ia ni hatari sana..

  Sasa nambie ikiwa Ulaya wenye utamaduni wa maintanace wanaihofia gas majumbani itakuwaje sisi Wadanganyika ambao hata bomba la maji tu tunashindwa kuli maintain?. Je, watakufa wangapi hali hata zima moto yenyewe shida...Moto wa gas tunaujua? huu ukianza nyumba moja utafuata bomba hadi bomba na pasipo immidiate respond unaweza kuondoa mji mzima. Sisi tumejiandaa vipi? kwa nini tusiendelee kutumia gas za mitungi ambazo ni safe zaidi kuliko kuweka mabomba ya gas ambayo walalahoi wanaweza kuyang'oa wakifikiria biashara ya chuma cha shaba?. Kosa la mtu mmoja au nyumba moja kusababisha vifo wa mamillioni ya watu?..

  Nitaendelea.....
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Aug 3, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Fursa za Maendeleo:-

  Profesa nitaendelea kuichambua hotuba ya rais kwa kutazama sio tu ubovu wa mikakati aloipanga bali pia sera nzima inayolenga kuyanufaisha mashirika ya nje na sio wananchi kwa sababu mikataba yote iliyotangulia haimnufaishi mwananchi na sintotegemea mashirika yale yale ya uchimbaji tuwe na sheira mbili tofauti ktk ubia ua masharti ya uwekezaji nchini..

  Kwa hiyo hatukuwa na maandalizi toka mwanzo, ila leo ndio tunaandaa Chuo kikuu cha Dar es Salaam kutoa mafunzo ya Uchimbaji wakati tuliwanyima fursa hizo wanafunzi wale waliokuwa wamefundishwa toka wakati wa Nyerere. Halafu Siku zote wenyetu huzuia uchimbaji kuanza hadi wasomi wake wameisha hitimu na tayari kuanza kazi leo sisi tumeshagawa tayari contract za Uchjimbaji halafu ndio tunasema... Hatuwezi kuingia mikataba mibovu wakati tukiwasomesha vijana wetu halafu miaka mitano baadaye wakirudi ndio waje sijui kurekebisha mikataba au kupewa ajira..

  Kama Kweli serikali yetu inategemea Gas na Mafuta kuleta mabadiliko nchini basi tuishie tu kwenye Upatikanaji wa gas na Mafuta.. Tusiweke mkataba na nchi yoyote kuhusu Uchimbaji hadi wataalam wetu wahitimu.. Hili ni jambo ambalo nija hakaika haliwezekani na wala JK sii mtu wa subira hivyo..Tutaingizwa ktk mikataba mibovu tukitegemea zaidi kuwapoatia Ajira kwa vijana wetu.... Hii nchi yetu imeshauzwa na maneno haya ya JK mwishoni:-

  "Mambo hayo tumeshaanza kuyafanyia kazi. Katika mazungumzo yangu na baadhi ya wakuu wa nchi rafiki na mashirika ya maendeleo ya kimataifa, nimewasilisha maombi ya kusaidiwa na kushirikiana kwa mambo mawili. Kwanza kwa kuwawezesha Watanzania kupata mafunzo ya haraka kwa wataalamu watakaosaidia kusimamia shughuli za utafutaji, uendelezaji na biashara ya gesi asili nchini.
  Pili, watusaidie kupata watu wenye ujuzi na uzoefu ili watushauri kuhusu namna ya kutengeneza mifumo bora ya kusimamia na kutumia mapato ya gesi kwa mujibu wa mifano ya wenzetu waliofanikiwa. Nafurahi kwamba maombi yetu yamepokelewa vizuri na nchi zote na mashirika yote ya kimataifa tuliozungumza nao. Baada ya muda si mrefu kazi itaanza."  Kauli hii imefuta umuhimu wa fursa zote alokuwa akizizungumzia kwa sababu Mbwa kajipeleka kwa Chatu...Japokuwa nina hakika Wadanganyika wengi hawaamini hili..AFRICOM ipo kazini na watahakikisha tunatawaliwa kiuchumi ka makosa kama haya. Ni ajabu sana kwa nchi maskini kuwafuata WANYONYAJI kuomba ushauri au msaada kwa kitu ambacho wanakitafuta kwa nguvu zote hadi kutangaza vita..Mawazo kaa haya yanatueleza mengi sana ya kwamba hatupo tayari kabisa kuingia biashara hii kwa sababu huwezi kwenda kumuomba msaada MNYONYAJI...
   
 6. c

  chama JF-Expert Member

  #6
  Aug 3, 2012
  Joined: Aug 6, 2010
  Messages: 8,006
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Mkandara;
  Wakati wa Mwalimu tulikuwa na chuo cha madini Dodoma sijui kama bado kipo; kitu muhimu ni kuwa na mikataba yenye tija kwa taifa wataalamu tunaweza kuanza na wa nje wakati tukisomesha wataalamu wetu tunahitaji hizi rasimali kuboresha maisha ya watanzania.

  Chama
  Gongo la mboto DSM
   
 7. M

  Mkandara Verified User

  #7
  Aug 4, 2012
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Nakubaliana na wewe sana tu lakini huwezi kufanya Exploration toka mwaka 1992 hujapeleka wanafunzi kujifunza ila leo ndio tunafikiria wakati visima hugundiliwa kila baada ya miaka na uchimbaji tayari umeshaanza.. Halafu Hotuba nzima hadi leo hii haikuzungumzia kabisa ni kiasi gani cha hisa sheria yetu itawalazimisha wawekezaji. Watanzania wapo kizani hadi leo ukiuliza kwa nini tuna mashatri mepesi hivyo watakujibu tukiwabana hawatakuja wekeza nchini?... Hivi ni nani alowaambia maneno haya? kwamba tukiwadai share wataondoka! Hawa watu wanaishi kwa kutegemea rasilimali zetu, rasilimali zetu ndizo ndio mkate wao mezani, ndio picha ya puto unaloliona ktk masoko huria, Hivi kweli mnafikri tukiwanyama watakwenda wapi kuipata gesi kwa urahisi ama yenye mikataba laini?.. WAPI..

  Ukweli ni kwamba hakunanmahala watakwenda ipata dhahabu kama yetu, hakuna mahala watakwenda ipata gesi kama yetu na tukiwanyima siku hiyo hiyo bei ya dhahabu inapanda soko la dunia na pengine shirika kufa.. Barricks inaweza ku collapse kesho soko la TSE au NYE tukiwaondoa Tanzania. Sasa ni nani anamhitaji nani zaidi?. Wakitishwa kidogo tu wanafungua nadi limango ya vyumbani... Kuna wakati husema nadhani ipo haja ya Nchi za Kiafrika kumpata rais aliyewahi kuishi nchi za nje anayefahamu wazungu wanafikiria nini na wanaweza kufanya nini hasa pale wanaposema - FOR THE INTEREST OF MY COUNTRY. Maneno haya yana impact gani ktk maamuzi ya viongozi au rais wao na anawajibika kuyatukuza kwa kiasi.
   
Loading...