President Magufuli , CCM just say sorry to Tanzanians

viking

JF-Expert Member
Aug 23, 2012
1,702
2,000
Kiongozi bora ni yule anaeomba msamaha kama makosa yametokea ili watu wazidi kusonga mbele. Hii issue ya ACACIA , hakuna hata kiongozi mmoja wa CCM atakae simama hadharani na kuomba msamaha kwa Watanzania .

Zimeundwa kamati zaidi ya 6 pamoja na mapendekezo kutolewa lakini hakuna hata kamati moja mapendekezo yake yaliopokelewa kwa utekelezaji. Hii leo mnakalia kuwapiga vijembe wapinzani kwamba wamepewe hela na wanawatetea ACACIA .

Watanzania wa leo wamebadilika na tunajua ukweli uko wapi.Mheshimiwa rais acha kuwatisha wapinzani ,busara na hekima ndio zinazotakiwa kipindi hiki.

Wapinzani kilio chao siku zote ni mikataba iletwe bungeni ijadiliwe , Serikali yako siku zote imekuwa ikipitisha hoja za dharura ambazo zina maslahi ya Taifa bila kujadiliwa vizuri bungeni.

Tusingefika hapa kama mapendekezo ya kamati zote za nishati na madini yangepewa kipaumbele
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom