President Jakaya Kikwete flies to Addis Ababa..!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

President Jakaya Kikwete flies to Addis Ababa..!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Mar 9, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  [​IMG]
  The Chairman of the African Union Commission (AU) Jean Ping welcomes to Addis Ababa President Jakaya Mrisho Kikwete shortly after he arrived at Bole International airport for a special summit on Ivory Coast Crisis (Photo by Freddy Maro)


  There is a communication vacuum and the result is hyped up perceptions that are influencing peoples actions. This is not good at all!It could result in the wrong actions being taken leaving bitterness and anger in its wake.These are two feelings you do not want to contend with as a leader. People need to know the true facts so they can filter the real from the chaff.
   
 2. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #2
  Mar 9, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 897
  Trophy Points: 280
  hawezi rudi nyumbani mpaka apate mgawo wake wa dowans.

  ndo maana aliondoka na mshrika mwenzake (ngeleja) kwenda paris. najua watakuwa wamekutana na RA, brigedia na wadau wote wa dowans.
   
 3. kapotolo

  kapotolo JF-Expert Member

  #3
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 19, 2010
  Messages: 3,727
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Du Jamaa siku hizi hata haagi, kimya kimya tu mtamkoma, halafu anawahi hata mwenyekiti hajafika, sijui alihonga achaguliwe mjumbe kwenye hii nafasi, anaifanyia kazi hasa. Lakini labda ni dalili ya kwamba kelele za mlango sasa zinamzuia mwenye nyumba kupata usingizi, anaenda kulala kwa Jirani.
   
 4. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #4
  Mar 9, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  His Excellency, Dr Dr Dr Al haj Mr President...
   
 5. samora10

  samora10 JF-Expert Member

  #5
  Mar 9, 2011
  Joined: Jul 21, 2010
  Messages: 6,644
  Likes Received: 1,436
  Trophy Points: 280
  utampenda kwenye ishu kama hizo..
   
 6. EMT

  EMT JF-Expert Member

  #6
  Mar 9, 2011
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 14,464
  Likes Received: 865
  Trophy Points: 280
  Duh! Lini tena hii?
   
 7. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #7
  Mar 9, 2011
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  Vasco da gama in his job!!
   
 8. Gurudumu

  Gurudumu JF-Expert Member

  #8
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2008
  Messages: 2,350
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI

  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete leo, Jumatano, Machi 9, 2011, anaungana na marais wenzake wa Afrika waliopewa jukumu la kutafuta suluhu ya mgogoro wa kisiasa katika nchi ya Afrika Magharibi ya Ivory Coast, katika hatua za mwisho za jitihada za kujaribu kumaliza mgogoro huo.

  Rais Kikwete na marais wenzake wanakutana mjini Addis Ababa, Ethiopia, katika jitihada mpya za kutafuta jawabu la mzozo huo uliolipuka mwishoni mwa mwaka jana kufuatia matokeo ya raundi ya pili ya uchaguzi wa Rais wa nchi hiyo uliofanyika Novemba 28, 2011.

  Katika mkutano huo wa siku mbili, marais hao wanatarajiwa kukabidhi ripoti yao kwa Kamati ya Amani na Usalama ya Umoja wa Afrika (AU), ili kuuwezesha Umoja huo kuchukua uamuzi kamili wa jinsi ya kumaliza mgogoro huo.

  Ripoti hiyo ni matokeo ya mikutano ya marais hao mjini Addis Ababa, huko Mauritania ambako walikutana mara mbili, na mjini Abidjan, Ivory Coast. Marais hao waliteuliwa na Kikao cha Wakuu wa Nchi Wanachama wa AU katika mkutano wao wa Januari mwaka huu.

  Rais Kikwete ameondoka nchini leo asubuhi kwenda Ethiopia kwa kikao hicho cha siku mbili ambako ataungana na Rais Jacob Zuma wa Afrika Kusini, Rais Idriss Deby wa Chad, Rais Blaise Campaore wa Burkina Faso na Rais Mohamed Abdel Aziz ambaye ni mwenyekiti wa kundi hilo.

  Wengine wanaotarajiwa kushiriki katika kikao hicho ni Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AU) Bwana Jean Ping na wawakilishi wa Jumuia ya Uchumi ya Afrika Magharibi (ECOWAS) na Umoja wa Mataifa (UN).

  Mzozo wa Ivory Coast ulianza baada ya taasisi mbili zinazosimamia uchaguzi nchini humo kutangaza matokeo tofauti ya washindi wa raundi hiyo ya pili ya upigaji kura kati ya Mheshimiwa Laurent Gbagbo, aliyekuwa anatetea kiti chake na mpinzani wake mkuu, Mheshimiwa Alassane Quattara.

  Tume ya Uchaguzi ya nchi hiyo ilimtangaza Quattara kuwa mshindi wa uchaguzi huo kwa asilimia tisa, lakini siku nne baadaye, Baraza la Katiba la nchi hiyo lilimtangaza Gbagbo kuwa mshindi kwa asilimia moja.

  Baraza hilo lilimtangaza Gbagbo mshindi baada ya kuwa limefuta matokeo katika majimbo saba aliyokuwa ameshinda Quattara, kaskazini mwa nchi hiyo ambako ndiko ngome kuu yake ya kisiasa. Kwa kufuta matokeo katika majimbo hayo, Baraza lilimpunguzia Quattara kura 600,000.

  Tokea wakati huo, viongozi hao wawili wote wamejitangaza marais na kila mmoja kuunda Serikali yake. Nchi hiyo sasa imetumbukia katika mgogoro kamili wa kisiasa na vita ya wenyewe kwa wenyewe ambako yamekuwepo mauaji ya watu na uharibifu mkubwa wa mali nchini humo.

  Imetolewa na:

  Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,

  Ikulu

  DAR ES SALAAM  09 Machi, 2011
   
 9. m

  mob JF-Expert Member

  #9
  Mar 10, 2011
  Joined: Dec 4, 2009
  Messages: 2,028
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  ivi hii safari inagarimiwa na nani
   
 10. nziriye

  nziriye JF-Expert Member

  #10
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 23, 2011
  Messages: 960
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 45
  bon voyage mr president,ingekuwa vyema kama ungeenda kimya kimya mana safari zako zinakera masikioni mwa wa-tz weng.
   
 11. Watu

  Watu JF-Expert Member

  #11
  Mar 10, 2011
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 3,054
  Likes Received: 427
  Trophy Points: 180
  Mbona Paris alikwenda kimya kimya? au kurugenzi ya mawasiliano ikulu haikuona umhimu wa kutoa taarifa?
   
 12. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #12
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,903
  Likes Received: 5,365
  Trophy Points: 280
  ndani ya siku 100 kaenda nje mara 5,..piga hesabu kwa miaka 5 atasafiri mara ngapi??tushamzoea na aibu hana huyu jamaa duh!!
   
 13. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #13
  Mar 10, 2011
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  Hivi ukichaguliwa kwenye kamati huwezi kukataa..? bwana mkubwa punguza safari shughulikia wapiga kura wako kwanza..
   
 14. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #14
  Mar 10, 2011
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kwa wenzetu mtu kama huyo anaitwa Roving Ambassador lakini hapa kwetu tunamwita Mtukufu Raisi, ni tafsiri tu!
   
 15. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #15
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  hata Loliondo kwa Askofu nako ilikuwa kimya kimya
   
 16. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #16
  Mar 10, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  vp kaenda kutalii?
   
 17. R

  Rangi 2 Senior Member

  #17
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 171
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Anadhani kuwa yeye bado ni waziri wa mambo ya nchi za nje na ushirikiano wa kimataifa....
   
 18. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #18
  Mar 10, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Anaogopa kukaa nyumbani kusikiliza matatizo ya wananchi; Ni bora kwenda nje na kula vizuri
   
 19. Kamkuki

  Kamkuki JF-Expert Member

  #19
  Mar 10, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 1,067
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 145
  hata kama inawezekana lakin sio kwa Mkwere!!
   
 20. n

  niweze JF-Expert Member

  #20
  Mar 10, 2011
  Joined: Oct 21, 2009
  Messages: 1,008
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mbona hakutani na wananchi wa Gongo la Mboto na watanzania wengi wasio na umeme?
   
Loading...