President aonesha udhaifu wa Waziri mkuu hadharani, hii imekaaje jamani?

Mwanamayu

JF-Expert Member
May 7, 2010
11,609
6,823
President asema zaidi ya mwaka mmoja tangu PM ashike wadhifa huo hakufahamu kama kuna sheria inasema PM ni mwenyekiti wa baraza la kudhibiti madawa ya kulevya. "Kama anajua, amejua jana au leo". Na akaenda hatua moja mbele kusema hata wajumbe ambao ni mawaziri hawakuwa na habari hiyo.

Je, na PM na mawaziri wake wafuate spirit hiyo ya "lazima tuwe wakweli, tusijifanye malaika kwa kuficha ukweli"?

=====

Dar es Salaam. Rais John Magufuli amesema Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alikuwa hajui kama yeye ni Mwenyekiti wa Baraza la Kudhibiti Dawa za Kulevya kama ilivyobainishwa kwenye sheria.

Rais Magufuli amesema hayo wakati akiwaapisha viongozi mbalimbali, Ikulu na kuagiza wakachape kazi bila kumuogopa mtu yeyote.

“Kama anajua, amejua jana au leo. Nina uhakika hata mawaziri wake ambao ni wajumbe wa baraza hilo walikuwa hawana taarifa na hakuna aliyewakumbusha,” amesema Rais na kuongeza: “Hata mimi sikuletewa mapendekezo ya kumteua kamishna mkuu wa mamlaka hii (ya Kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya, Rogers Sianga). Nilimteua kwa sequence (utaratibu) niliyonayo mwenyewe. Lazima tuwe wa kweli, tusijifanye malaika kwa kuficha ukweli,” alisema Rais Magufuli.

Pia, ameeleza kuchukizwa na kitendo cha watu kwenda Kituo Kikuu Polisi (Central) na kuanza kuosha gari la mtuhumiwa huku wengine wakienda na kwaya katika eneo hilo.

Tukio hilo lilitokea Alhamisi iliyopita wakati mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji alipokwenda kuripoti polisi na baadhi ya mashabiki wake kuosha gari lake lililokuwa limeegeshwa katika kituo hicho.

Wengine wanaoaminika kuwa ni wanakwaya wa Kanisa la Ufufuo na uzima linaloongozwa Askofu Josephat Gwajima walifika eneo hilo wakati kiongozi wao alipokwenda kuhojiwa huku wakiimba nyimbo mbalimbali.

“Sitaki kuona tena wananchi wanajazana kituo cha polisi watuhumiwa wanapohojiwa. Lazima tujenge nidhamu, mbona hawakwenda Lugalo kwa CDF (Mkuu wa Majeshi) kuimba kwaya?” amesema Rais Magufuli huku akimuagiza Kamishna wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Simon Siro.

Chanzo: Mwananchi
 
Sio hivyo tu kabla ya kuongea Rais alimpa nafasi Ndugu Kassim aseme chochote ambapo katika hotuba yake alitaja idadi ya watanzania waliofungwa nchi za nje..Lakini kuonyesha kwamba Ndugu Majaliwa hakufanya utafiti wa kutosha idadi aliyoitaja ilitofautiana sana na aliyotaja JPM.. Alidhalilika sana PM
 
Wameteuliwa na mh rais lakini hawakupewa job description yaani ministerial instruments ...wote hawakupewa na hawajapewa ....muulize Zitto
Wakati wanaambiwa jambo hilo kule bungeni ilionekana kama lisilo na maana kwa vile limesemwa na wapinzani lakini ndio ukweli kwani kama Waziri mkuu anakaa mwaka mzima na hajui baadhi ya majukumu yake basi hiyo serikali ni ya ajabu sana
 
Kwanini leo Waziri Mkuu ama Waziri wa Mambo ya ndani hawakuongoza ule mkutano wa kuhusu madawa ya kulevya badala Makonda ndio alikuwa mgeni rasmi.
Wewe utakuwa hujui nchi hii baada ya jpm kimamlaka anafuata nani! Kuna watu huwa wananyang'anywa madaraka bila kutangazwa na wakinyamaza kama alivyofanya pm wetu hali inaendelea hivyo hivyo. Waliokuwepo kipindi cha Mrema akiwa waziri wa mambo ya ndani wanakumbuka alipopewa cheo kisichokuwepo kwenye Katiba cha naibu waziri Mkuu wanajua aliyofanya. Mara nyingi watoto watukutu wakisifiwa wana mbio hukimbia mpaka wanapitiliza nyumbani kwao.
 
Duh! Yaani Rais wa nchi alikuwa hafahamu wakati mimi niliye mtaani tu nilikuwa nalifahamu hilo tangu kitambo!!! No wonder aliwateua akina Bulembo wakati alikuwa ameshateua wabunge wanaume 4!! Inawezekana nalo hakufahamu!!
 
Sio hivyo tu kabla ya kuongea Rais alimpa nafasi Ndugu Kassim aseme chochote ambapo katika hotuba yake alitaja idadi ya watanzania waliofungwa nchi za nje..Lakini kuonyesha kwamba Ndugu Majaliwa hakufanya utafiti wa kutosha idadi aliyoitaja ilitofautiana sana na aliyotaja JPM.. Alidhalilika sana PM

Magu ni mtaalum wa kutunga takwimu.
 
Wameteuliwa na mh rais lakini hawakupewa job description yaani ministerial instruments ...wote hawakupewa na hawajapewa ....muulize Zitto

Kama MAGUGU anaona MAKONDAKTA ndiye anajua kutawala bila ya Instrument si ampe huo UWAZIRI MKUU na ampige chini MAJALIWA NA baraza lote la Mawaziri. Kama vipi turudi kwenye Ballot Box tena. Shida ni gani???
 
Wakati wanaambiwa jambo hilo kule bungeni ilionekana kama lisilo na maana kwa vile limesemwa na wapinzani lakini ndio ukweli kwani kama Waziri mkuu anakaa mwaka mzima na hajui baadhi ya majukumu yake basi hiyo serikali ni ya ajabu sana
Tena sanaaaa
 
Nafikiri ni udhaifu wa ofisi ya waziri kiongozi na zaidi ofisi ya waziri mkuu mwenyewe.

Ofisi ya waziri mkuu, kwa maoni yangu, inapaswa ijue mamlaka na nyadhifa zote za waziri mkuu. Ofisi ya katibu kiongozi hali kadhalika!

Je, kwa namna fulani ni kama alikuwa amerusha dongo kwa watangulizi wake (JK, Sefue)?

Lakini pia inaonesha udhaifu mkubwa sana kwenye mapambano dhidi ya madawa ya kulevya. Kama tangu 2015, sheria ipo lakini haikupewa uhai maana yake nini? Muda wote huu walikuwa wanapambana kwa kutumia instrument gani?
 
Back
Top Bottom