Presha yangu inasoma 165/110..Naombeni ushauri

kikaniki

JF-Expert Member
Nov 20, 2014
508
962
Kwa takribani miezi miwili sasa nimekuwa nikijihisi tofauti. Mapigo ya moyo wangu yamekuwa yakienda kwa kasi.

Leo nikaamua kwenda hospitali kupima.

MAJIBU:-
* Blood Pressure = 165/110
* Uzito = 86Kg
* Urefu = 175 cm

Daktari kaniambia Presha hiyo sio nzuri.

kanishauri nipunguze matumizi makubwa ya chumvi katika chakula.

Ninaomba ushauri mwingine kwa wenye ufahamu na utaalamu.

NB: Sinywi pombe wala sivuti sigara
 
kikaniki dawa ya magonjwa mengi ni mazoezi,halafu lazima uwe na nidhamu ya kula yaani asubuhi kula sana,mchana kidogo halafu jioni juice au hata chai tu
 
Nina miaka 39 ndugu
Unaweza kupitia chati hapa chini ujue unapaswa kuwa na msukumo wa damu kiasi gani, baadae nitarudi kwa ajili ya maswali na ushauri.

uploadfromtaptalk1463564108602.jpeg
 
Usipende kuchanganya madaktari kwa wakati mmoja. Kuwa na Dr mmoja at a time. Wapishi wengi huharibu mchuzi!!
 
1. Kwa umri wako tizi linakuhusu sana hata kama ni kutembea kwa saa kila siku.
2. Lishe; punguza chumvi, mafuta (sp. animal fats), wanga (hasa mlo wa usiku), ongeza matunda na mboga za majani, binafsi matango, mdalasini na asali ni msaada sana kwangu.
3. Uhusiano kati ya uzito na urefu wako (BMI) sio rafiki hivyo pambana upunguze japo 8kg.
Mimi hali ilikua mbaya zaidi .. Kwa sasa niko vzr .
 
Shukrani sana kwa ushauri wako. Nitazingatia yote
 
Back
Top Bottom