Pres Jakaya Kikwete, You have made us proud!

Pres Jakaya Kikwete, You have made us proud!

Indeed my friend, if the Prez. stands high today, it is because he stands on the shoulders of those who have gone before him! Let's wait and see how high those who will follow him will reach by standing on his shoulders when he is done and gone.
 
Hizi tabia za kusubiria Misiba ndo watu watokelezee ni za kichawi sana aisee.
Tumeona mifano mingi ya misiba ya wans Bongo Movie.
Ptuuuuuuu....
 
Ndugu zangu,

NOTHING can come from NOTHING. Wamesema hili Wanafalsafa wa Uyunani ya Kale .

Nimemwona na kumsikiliza Rais wetu Jakaya Kikwete akizungumza kwenye siku muhimu ya kumuaga kwa mara ya mwisho Mzee wetu Nelson Mandela.

Muda wote wa hotuba yake, JK alibaki kwenye mstari kwa namna ile ile ya kuweka bayana kwa ulimwengu, kuwa ' msione vinaelea'.

Hakika alichofanya JK leo ndicho haswa alipaswa kukifanya, na amekifanya kwa kutumia weledi wake kwenye diplomasia na kuchanganya uzoefu wake kwenye uongozi wa kisiasa na dola kwa ujumla.

Ni kuitumia fursa ile ambapo macho na masikio ya dunia yalielekezwa Quni, kwa yeye rais kuiambia dunia, na si kuisubiri CNN au vyombo vya habari vya Kimagharibi kuifanya kazi hiyo, juu ya mchango wa Tanzania katika harakati za ukombozi wa bara la Afrika ikiwamo mchango wa Tanzania kumfanya Mandela na viongozi wengine wa Kiafrika kuonekana kama walivyoonekana kwenye macho ya dunia.

Hakika, JK anastahili pongezi kwa kazi njema aliyoifanya leo ya kuiweka tena Tanzania katika ramani ya dunia, si tu kama nchi ile ya mbuga za wanyama na Mlima Kilimanjaro, bali ' Taifa Kubwa' lililochangia kushiriki mikakati ya ukombozi ikiwemo kutoa misaada ya silaha, mafunzo na hata makazi kwa wapigania ukombozi wa Afrika.

JK aliipitia historia ya mchango wa Tanzania ambayo wengi waliokuwa wakimsikiliza, ama waliisahau au hawakuijua kabisa.

Lakini, tujiulize pia kama Watanzania, katika aliyoyasema JK kule Quni, ni Watanzania wangapi wanayajua? Inahusu umuhimu wa kuipitia historia yetu ili, kama Watanzana, tuweze kumiliki ' K3'- Kujitambua, Kujiamini na kuthubutu. Imefika mahali tunaionea aibu hata historia yetu.

Na nyongeza katika yale aliyoyasema JK leo ni kumbukumbu ya kihistoria ambayo haitajwi pia, kuwa Baba wa Taifa , Mwalimu Nyerere, ndiye aliyempa hifadhi Tanzania, Rais wa Pili wa Afrika Kusini huru, Thabo Mbeki baada ya kutoroka Afrika Kusini. Baadae Thabo Mbeki akaenda kusoma Uingereza.

Jambo hilo linathibitishwa katika kitabu alichoandika msomi mahiri wa Afrika Kusini, William Gumede. Anasema;

" In 1962, Thabo slipped out of the country to which he would not return for twenty -eight years, travelling through Botswana to Rhodesia, where he was arrested and held in a Bulawayo prison for several weeks. The white Rhodesian authorities intended to deport him back to South Africa and waiting for security police, but British Labour MP, Barbara Castle intervened after being lobbied by the ANC, and Mbeki was granted asylum in Tanzania by President Julius Nyerere." ( William Gumede, Thabo Mbeki and The Search For Soul of The ANC, pg 36)

Naam, ni wakati sasa wa viongozi wengine, bila kujali itikadi zao, wanapokuwa kwenye majukwaa ya kimataifa, kuzitafuta fursa za kuonyesha yale ambayo huko nyuma tumekuwa na uwezo nayo, na bado, kama nchi, tunaweza kuaminika katika kutoa mchango wa uzoefu wetu kwenye masuala mbali mbali ya Kimataifa.

Usiku Mwema.

Maggid Mjengwa.
Iringa.
 
Hizi tabia za kusubiria Misiba ndo watu watokelezee ni za kichawi sana aisee.
Tumeona mifano mingi ya misiba ya wans Bongo Movie.
Ptuuuuuuu....
Hebu tupe scenario mbadala mkuu, ilikuwa inajulikana nzee Madiba anaugua na wakati wowote anaweza kufariki.
Tupe mambo ambayo yangeweza kufanika tofauti na ilivyofanyika sasa.

Wakati mwingine wivu unatuondolea hekima.
 
Akili zetu watanzania ovyo sana, tunasifia na kushangilia hotuba bora huku tukiwa na barabara mbovu, umeme mgao kila siku, hospitali hakuna madawa, shuleni mambo ovyo vitabu hakuna wala vifaa vya maabara, lakini tunashangilia eti Rais wetu katoa hotuba bora! Hiyo hotuba itasaidia ku-solve matatizo yetu???
Hebu tujifunze kufikiria kama binadamu wenye akili timamu basi! Inauma sana!
 
Maggid,

Mimi siyo supporter mkubwa wa huyu Raisi wetu lakini kwa hii hotuba ya leo amefanya vizuri. Let's call a spade a spade. The man was focused and sounded incredibly prepared. He was able to expose to the world what our country has done to liberate Africa without looking like he's bragging about it. Pia the fact kwamba amesafiri na watu wawili key kwenye hiyo speech yake (Mama Nyerere na Mama Nsilo) inaonyesha alikuwa na maandalizi mazuri na wale waliomshauri kwenye hii lazima wapewe kudos.
 
Akili zetu watanzania ovyo sana, tunasifia na kushangilia hotuba bora huku tukiwa na barabara mbovu, umeme mgao kila siku, hospitali hakuna madawa, shuleni mambo ovyo vitabu hakuna wala vifaa vya maabara, lakini tunashangilia eti Rais wetu katoa hotuba bora! Hiyo hotuba itasaidia ku-solve matatizo yetu???
Hebu tujifunze kufikiria kama binadamu wenye akili timamu basi! Inauma sana!

Kwani wewe hii post yako ya kiBavicha imesaidia kujenga barabara?
 
Nakuunga mkono ndugu Maggid. Hotuba ilikuwa nzuri na ina historia nzuri ambayo nadhani wengi wetu hatukuijua yote. Thanks kwa hili kutoka kwa JK. Ni vizuri kwa watanzania ku appreciate mazuri yanayofanywa na wenzetu kuliko kila wakati kudharau na kukejeli kila kitu. Wenzetu hasa ukiangalia ulaya wanathamini sana michango ya wenzao ndiyo maana katika maeneo mengi wanaweka sanamu na hata kuandika vitabu kuhusu mashujaa mbalimbali katika taifa husika. Kwa kufanya hivyo wanasaidia kuzalisha vizazi vinavyopigania kufanya mazuri na hivyo kuendeleza nchi hizo.
 
Sure maggid. Kwa kweli ni hotuba iliyoandaliwa vyema nampa pongezi kwa hilo ingawa ingawa anamadhaifu yake.
 
alishindwa kuunganisha ni jinsi gani viongozi wa africa wanaweza kumuuenzi mandela kwa vitendo, na sio maneno matupu, ndio tanzania ilimsaidia lkn na yeye kama rais anafanya nini hasa kuiga misingi aliyosimamia mandela hasa ktk kuleta maendeleo kwa watu wake, kuondoa ufisadi, kuwa na utawala unaosimamia katika kweli?
 
Back
Top Bottom