Precision Air yakanusha taarifa zinazodai wako mbioni kufunga virago na kufukuza baadhi ya wafanyakazi kutokana na athari za janga la COVID-19

Cannabis

JF-Expert Member
Jan 20, 2014
8,938
25,282
Shirika la ndege la Precision Air limekanusha habari iliyochapishwa na Sauti kubwa tarehe 29/12/2020 yenye madai ya kwamba kutokana na athari za janga la COVID-19 shirika hilo, lipo mbioni kuacha kufanya biashara katika robo ya kwanza ya mwaka 2021, kuachisha kazi marubani 50 na kwamba hivi sasa shirika hilo lina ndege mbili tu zinazofanya kazi.

Shirika hilo limewahakikishia wateja wake kuwa lipo katika hali nzuri ya kibiashara na kuishukuru serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa mchango wake mkubwa katika usafiri wa anga, na kuwezesha sekta ya utalii kuendelea kufanya kazi katika kipindi ambacho dunia inakabiliana na janga la COVID-19.

Pia shirika hilo limesema lina ndege 11 zinazofanya safari Dar es Salaam, Arusha, Bukoba, Dodoma, Kahama, Kilimanjaro, Mbeya, Mtwara, Mwanza, Zanzibar na Nairobi.

EqfWONRUUAExMLQ.jpg
.​
 
Kwani Wangesemaje Kuhusu Hilo!!!
Tuwape Muda Tu, Baadaye Business Digenda Shoti
😀😁😂🤣😃😄😅😍😃🤣😂😁😆😅😄😃🤣😀😁😁
 
Tumesafiri nao kutoka dar to mwanza..tulikuwa only abiria 9.sasa sijui kama wanapata faida kweli hawa
 
Back
Top Bottom