Ndege ya Air Tanzania yashindwa kutua Bukoba, yageuza kwenda kutua Mwanza

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
25,492
54,890
Ndege ya Air Tanzania imeshindwa kutua Bukoba Airport imerudi Mwanza.

Stay tuned



======

UPDATES

Ndege ya Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) imeshindwa kutua katika uwanja wa ndege wa Bukoba mkoani Kagera kutokana na hali mbaya ya hewa. Badala yake ndege hiyo imelazimika kutua salama katika uwanja wa Mwanza.

Alipoulizwa kwa simu leo Alhamisi Novemba 17 kuhusu tukio hilo, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA), Hamza Johari amethibitisha tukio hilo.

“Ni kweli nimepata taarifa ndege ya Air Tanzania imeshindwa kutua kutokana na hali mbaya ya hewa, kulikuwa na ukungu, mvua, radi na giza uwanja ukawa hauonekani, kwa hiyo rubani akafuta safari na kurudi Mwanza na ametua salama,” amesema.

Awali taarifa iliyotumwa na Mbunge wa Viti Maalum, Neema Lugangira kwenye mitandao ya kijamii ilieleza tukio hilo.

“Still shaken lakini Mungu ni Mwema. Nimepanda ndege asubuhi ya leo kwenda Bukoba. Safari ilikuwa na changamoto, tumefika lakini ndege ikashindwa kutua.

“Nampongeza rubani kwa uamuzi sahihi wa kurudi Mwanza na sasa narudi Dar. Serikali ibebe kwa uzito suala la airport mpya Bukoba,” ameandika.

Hali hiyo imejitokeza zikiwa zimepita siku 11 tangu ndege ya shirika la Precision ilipoanguka katika ziwa Victoria na kusababisha vifo vya watu 19 na wengine 29 wakaokolewa.

Chanzo: Mwananchi
 
Ni kawaida sana hiyo kwenye ndege..kuna siku ndege ya usiku tulikua tumetoka Dar to mwanza na fastjet ile ndege ya mwisho saa nne usiku ilishindwa kutua mwanza airport sababu mvua na hali ya hewa,tukarudi Dar tena.

Baada ya kama 3 hours tukaamsha tena kwenda mwanza..tulifika almost kunakucha . Nilijuta sana kupanda ndege ya mwisho
 
Yule rubani wa ndege iliyoanguka angefanya kama huyu angeepusha ile ajali, haya matukio ni ya kawaida hasa hali ya hewa inapokuwa hairuhusu kutua uwanja uliokusudiwa.
 
Kawaida sana kwa sisi marubani hio ni uamuzi sahihi sio kulazimisha kutua hata kama kuna ugumu
Mkuu wewe basi rubani muoga. Mimi ndio zangu hizo hasa naporusha hivi vi cassena single engines. Nimeshawahi kutua kwenye hurricane Bahamas.

Pia nimeshawahi kutua kwenye tornado texas. Nimeshawahi kutua kwenye dhoruba ya monsoon India. Nimeshawahi kutua kwenye typhoon manilla ufilipino.

Nimeshawahi kutua kwenye snow storm (blizzard) Reykjavik Iceland.

Nimeshawahi kutua kwenye tropical cyclone Msumbiji tena hizi hizi single engines cassena.
 
Back
Top Bottom