Siku moja nilikuwa nasafiri kutoka Musoma Kuja Dar es salaam nikiwa na mtoto mdogo. Nilitegemea kuondoka saa kumi jioni cha ajabu masaa mawili kabla ya safari nikapigiwa simu eti niwahi Musoma airpot kuna COASTER (gari) yao inatupeleka tukapandie ndege Mwanza badala ya Musoma eti ndege ya Musoma ina matatizo. Tulisafiri kwa Coaster (gari) yao umbali wa zaidi ya km 200 huku nikiwa na mtoto mdogo dereva akikimbiza gari kwa speed kali ili awahi ndege ya saa kumi na mbili.Ki ukweli nilifika Dsm nikiwa nimechoka tena nikiwa frustrated nikaona kama mambo yenyewe ndiyo yale basi ni bora hata ukasafiri na basi maana utakuwa umeokoa transport cost.Kiukweli kama ningekuwa na muda wa kutosha ningewapeleka mahakamani ili wanilipe fidia kwani ukweli ni kwamba nililipa nauli ya ndege kutoka Musoma hadi Dar lakini wao wakachanganyia na Coaster (gari) yao katikati pia walinipotezea muda wangu kwani sikufika kwa muda muafaka.Hii imekuwa ni tabia yao kwani hata rafiki yangu yalimkuta pia.
Wadau huu ni uungwana kweli?