Precision air ni wababaishaji | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Precision air ni wababaishaji

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by JUMONG, Jul 18, 2012.

 1. J

  JUMONG Senior Member

  #1
  Jul 18, 2012
  Joined: Sep 16, 2011
  Messages: 107
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Siku moja nilikuwa nasafiri kutoka Musoma Kuja Dar es salaam nikiwa na mtoto mdogo. Nilitegemea kuondoka saa kumi jioni cha ajabu masaa mawili kabla ya safari nikapigiwa simu eti niwahi Musoma airpot kuna COASTER (gari) yao inatupeleka tukapandie ndege Mwanza badala ya Musoma eti ndege ya Musoma ina matatizo. Tulisafiri kwa Coaster (gari) yao umbali wa zaidi ya km 200 huku nikiwa na mtoto mdogo dereva akikimbiza gari kwa speed kali ili awahi ndege ya saa kumi na mbili.Ki ukweli nilifika Dsm nikiwa nimechoka tena nikiwa frustrated nikaona kama mambo yenyewe ndiyo yale basi ni bora hata ukasafiri na basi maana utakuwa umeokoa transport cost.Kiukweli kama ningekuwa na muda wa kutosha ningewapeleka mahakamani ili wanilipe fidia kwani ukweli ni kwamba nililipa nauli ya ndege kutoka Musoma hadi Dar lakini wao wakachanganyia na Coaster (gari) yao katikati pia walinipotezea muda wangu kwani sikufika kwa muda muafaka.Hii imekuwa ni tabia yao kwani hata rafiki yangu yalimkuta pia.

  Wadau huu ni uungwana kweli?
   
 2. Nyati

  Nyati JF-Expert Member

  #2
  Jul 18, 2012
  Joined: Mar 6, 2009
  Messages: 2,050
  Likes Received: 384
  Trophy Points: 180
  Siyo uungwana hata hivyo wao wanaona kuwa wao wana haki zaidi ya sisi wateja, kuna siku moja niliwahi Mwanza Airport. Nikaelekezwa kuwa nisubiri kidogo, nikafanya kosa kusubiri baadaye wakaniruka kuwa nimechelewa. nashukuru MUNGU nilweza kushikilia HASIRA kwani yule aloniambia alikuwa amesepa ili muda ufike, nililazimika kusafiri kesho yake. Sikujua ni hatua gani nichukue
   
 3. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #3
  Jul 18, 2012
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,343
  Likes Received: 1,810
  Trophy Points: 280
  Airline industry in Tanzania inahitaji mapinduzi makubwa...tunasuasua sana na coverage bado haitoshi. Kuna mikoa ni ngumu sana kufikika kwa usafiri wa ndege
   
 4. bornagain

  bornagain JF-Expert Member

  #4
  Jul 18, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 3,389
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  Kwa wakazi wa Msoma ni bora tu Precision wawaambie ukweli kuwa hawana ndege ya kwenda huko maana sio siri sijawahi kusikia mtu amepandia Musoma halafu asilalamike.Mi nachoona Musoma Mwanza sio mbali sana ni almost masaa matatu na robo ili kuepusha usumbufu ni bora muwe mnapandia Mwanza
   
Loading...