Precision Air mnakera na kuudhi sana

Fereke

JF-Expert Member
Apr 13, 2011
270
753
Tafadhari hili Shirika limezidi mno kila mara kuahirisha na ndege zao kuchelewa kuondoka bila kutoa sababu za msingi.

IMG_7403.jpeg

Leo reporting time saa 10 alfajiri, kuondoka kuelekea Dodoma saa 11:50 asubuhi. Lakini mpaka muda huu hakuna ndege, kila baada ya nusu saa abiria wakiuliza wanasogeza mbele nusu saa.

Muda ukifika kimya, abiria wakienda kulalamika wanasogeza tena mbele nusu saa. Muda ukifika hakuna, saa hizi wamepeleka mpaka saa 2 asubuhi.

Ebu fikiria mtu mpaka anakata ticket ya ndege kwa gharama kubwa ina maana ana haraka na jambo la muhimu au dharura ikiwemo wagonjwa.

Fikiria abiria waliopo Dodoma Airport na wanasubiri tu, wengine wana safari za nje wanatakiwa kuunganisha flight inakuwaje?

Kuna wageni hapa kutoka nje ya nchi wanalalamika mno bila kupewa maelezi yeyote. Badilikeni hiyo ni kampuni binafsi haitakiwi kuwa kama Shirika la Umma.

Nimeleta hapa Ili ujumbe uwafikie wahusika haraka. Sijui namna ambayo nitawafikishia ujumbe kwa haraka waone ni hasara na athari kiasi Gani abiria wanapitia.

Wahudumu wanajibu tuu kutokana na sababu za kiuendeshaji mwisho wamemaliza.

Sent from my Infinix X626 using JamiiForums mobile app
 
Tz ndege zote ni za michongo hata huduma zao ni mbaya sana.
Abiria wa ndege hana tofauti na abiria wa Ngorika bus au Bembea bus.
Upumbavu sana nchi hii kila eneo.
 
Hao jamaa ndio kawaida (default) yao. Siku ukiona umesafiri kama ulivyo plan basi shukuru Mungu. Sijui mi ATR yao Ile imechoka?
 
Sijui Serikali isingekuwa imenunua ndege zake ingekuwaje.Hawa Precision wangetunyanyasa mno.
 
Bado mna panda precious?

Mna mioyo ya chuma kweli. Maana mpaka inafikia kuwa na tabia ya kuahirisha au kuchelewa Kila wakati maana yake ni nini.

Nadhani jibu unalo na bado mnang'ang'ania kuzipanda. Haya!
 
Bado mna panda precious?????
Mna mioyo ya chuma kweli. Maana mpaka inafikia kuwa na tabia ya kuahirisha au kuchelewa Kila wakati maana yake ni nini.........
Nadhani jibu unalo na bado mnang'ang'ania kuzipanda. Haya!
Unaweza kuta fundi maiko bado anaipiga nyundo huko gereji
 
Back
Top Bottom