Pre-mature husababishwa na nini?

Aine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,605
0
Nawasalimu wote!

Nina rafiki yangu amejifungua mara tatu pre-mature na kila anapojifungua mtoto hufariki muda mfupi, kwa kweli inasikitisha sana na inauma kiasi ambacho hakiwezi elezeka. Hivi hii husababishwa na nini? na je kuna tiba jamani ebu naombeni ushauri ili tumsaidie mwenzetu.

Najua maombi pia yanahitajika sana, lakini pia utaalamu unahitajika.
 
Churamagamba

Member
Dec 25, 2013
36
0
Mmmh! pole yake jaman, ngoja tuwasubil wataalam lkn asikate tamaa aendelee kuwaona wataalam mbalimbali, Mungu atamjalia tu.
 
ZeMarcopolo

JF-Expert Member
May 11, 2008
14,013
2,000
Premature maana yake mtoto amezaliwa kabla ya muda wake kufika, yaani kabla ya wiki ya 38-40.

Iwapo mtoto atazaliwa kabla ya wiki ya 35, mapafu yake huwa hayajakomaa kiasi cha kumudu maisha ya kawaida. Watoto wa namna hii hustahili kupewa huduma ya msaada ya kupumua ili waweze kuishi. Vilevile kabla hawajazaliwa mjamzito hutakiwa kuchomwa sindano ya kusaidia kukomaza mapafu mara tu zinapoonekana dalili za mtoto kuzaliwa premature au pale mjamzito anapokuwa na historia kama hii ya kujirudia premature.

Watoto premature wanakuwa katika mazingira hatari kwa sababu viungo vyao vinakuwa havijajiandaa kwa maisha ya nje. Kwahiyo ni lazima wawekwe chini ya uangalizi madhubuti wa wataalam mpaka inapothibitika kuwa wanaweza kumudu kunyonya na mifumo mingine kufanya kazi. Pia hatari ya damu kumwagika kwenye ubongo wao inahitajika kuzuiliwa kwa kuwapa vitamin K pamoja na kupima ubongokwa ultrasound.

Sababu kubwa inayosababisha watoto kuzaliwa premature huwa ni infection.

Mama mwenye historia kama hii anahitaji uangalizi wa karibu wa daktari bingwa wa wajawazito.

Poleni sana.
 
Akhy D

JF-Expert Member
Jun 10, 2013
365
500
Ili kupata ufumbuzi wa tatizo mimi nakushauri uende ukawaone madaktari bingwa wa magonjwa ya kina mama kwa sababu kuna maelezo mengi yatahitajika mfano;
-hizo mimba zinatoka katika umri gani
-Historia ya tatizo katika familia
-kipindi baina ya mimba moja na nyengine
Na mengine mengi pamoja na uchunguzi wa kidaktari
 
ahsante sana mkuu ZeMarcopolo kwa maelezo yako mazuri, watoto wawili wa mwisho alienda kwa madaktari ambao ni specialist wa wanawake na huyu wa mwisho alikuwa daktari specialist wa magonjwa ya wanawake Muhimbili ambapo tulikuwa na matumaini makubwa ya kupata mtoto lakini akajifungua na miezi saba mtoto amekaa wiki tatu tu akafariki so sad aisee, tumesikitika sana na inauma isivyoelelezeka!!!!
 
Aine

JF-Expert Member
Nov 1, 2010
1,605
0
Ili kupata ufumbuzi wa tatizo mimi nakushauri uende ukawaone madaktari bingwa wa magonjwa ya kina mama kwa sababu kuna maelezo mengi yatahitajika mfano;
-hizo mimba zinatoka katika umri gani
-Historia ya tatizo katika familia
-kipindi baina ya mimba moja na nyengine

Na mengine mengi pamoja na uchunguzi wa kidaktari
nimekupata Akhy D, hapo kwenye red i concur with you, anyway, God knows na this time itabidi akae muda mrefu kwa kweli kwani amekuwa akipata tatizo hilo baada ya miezi kadhaa ana conceive. Mimba hazitoki ila huzaliwa mtoto katika umri ambao mtoto bado anakuwa hajakomaa kitaalam, then anafariki!!!!!so sad
 
Mkempia

JF-Expert Member
Mar 5, 2013
1,142
1,500
ZeMarcopolo, naomba ufafanuzi hapo kwenye infection. Hivi kuna infection inaweza kusababisha premature??
 
Smartboy

JF-Expert Member
Nov 12, 2010
1,110
1,250
Sorry hili tatizo la,dadaz kutoa mimba linaweza kuchangia hii hali? kwa maana akiimgia kwenye ndoa
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom