"Pre-Form One" (???) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

"Pre-Form One" (???)

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by Sipo, Sep 13, 2009.

 1. Sipo

  Sipo JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2009
  Joined: Jul 25, 2008
  Messages: 2,146
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  Hivi hizi pre form one hapa nchini kwetu maana yake ni nini? Kwamba kiwango cha elimu kimeshuka au watoto wetu na wadogo zetu siku hizi ni vilaza kiasi kwamba wanahitaji kuzi-activate hizo akilia zao kila wakati ili wasifeli.?

  Nasema hivyo kwasababu wanafunzi wa darasa la saba wamehitimu darasa hilo wiki iliyopita lakini kesho tarhe 14 Septemba 2009 kuna wazzi wameshaanza kuwapeleka watoto wao kuanza Pre-form one

  Kwanini watoto wasijengewe utamaduni wa kujiamini kuliko kuwa-overload uku kwa kuwaweka busy kilka wakati au uko wanakwenda kupumzika

  Tukumbuke pia kuwa mtoto kufahamu kufanya kazi za nyumbani ni sehemu ya masomo na sio kumweka mtoto mezani na kwenye tuition centre kila wakati
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2009
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 309
  Trophy Points: 180

  Sipo unakumbuka mambo ya enzi zileeee, wakati hata hakuna kitu kinachoitwa tuisheni, pre-unit, baby -class, middle-class na madude mngine meeeengi!

  Kwa mtazamo wa haraka haraka utasema kwamba siku hizi hali ya uelewa wa watoto imeshuka, lakini kutokana na mabadiliko mengi ya kijamii na kiteknolojia, na ongezeko kubwa la watu, kumezaliwa mashindano makali sana ya fursa mbalimbali za maisha, likiwemo ndani suala la hizo pre-something.

  Akili za watoto wa saa zinakuwa occupied na mambo mengi ya starehe na uhuni, mambo ya meseji za mapenzi, tv, tarakilishi etc.hivyo ni lazima mwisho wa siku mtoto huyu anatindikiwa upande fulani.
   
 3. K

  Kibongoto JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2009
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 227
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Kama ni hivyo basi ni afadhali wakashinde huko tuition tu. Nyumbani jamaa wanawanyemelea sana hawa (watoto wa kike) waliomaliza la saba. Pia wengine wengi wanachokifanya majumbani ni upuuzi mtupu. Kazi hawasaidii zaidi ya kuangalia tv na kujiingiza ktk vitendo vya kihuni vijiweni. Kwa upande mwingine watoto ni muhimu wapumzike ila mazingira ya sasa ndio taabu mtupu. Ukisema mtoto umemwacha home apumzike baada ya mitihani ndio unaambulia matatizo tu. Kabla matokeo ya mitihani utasikia binti ana uja uzito.
   
 4. MaxShimba

  MaxShimba JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2009
  Joined: Apr 11, 2008
  Messages: 35,816
  Likes Received: 129
  Trophy Points: 160
  It is a new conduit of making money wakulu.
   
Loading...