Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 97,101
- 136,751
Nadhani wengi mmeshausikia huo mlio. Ni mlio ambao unatengenezwa kwa kukutanisha sehemu za juu na chini za mdomo (lips) na kuzifunga na hatimaye kuachia hewa iliyokusanyika kwa kuzifungua sehemu hizo kwa kutumia nguvu kidogo. Matokeo yake ndio huo mlio.
Sasa nilipokuwa dogo, mtaani nilikuwa nikiwaona wakubwa zangu wakipiga huo mlio pindi waonapo mdada ambaye amewavutia akipita barabarani. Walikuwa wakifanya hivyo ili kuvuta nadhari yake kwao (draw her attention).
Kuna wadada ambao hawakupenda kusikia huo mlio na kuna ambao walipenda. Sasa mimi sielewi asili ya huo mlio nini. Halafu ningependa kujua kama siku hizi bado hiyo tabia ipo. Wadada wa humu yameshawahi kuwatokea hayo ya kupigiwa ppsss ppsss? Na kama yamewahi kutokea ulijisikiaje? Ulichukia? Ulifurahi?
Nakaribisha michango yenu...