Ppsss psss....

Hommie huo nao unaweza kuwa MUKTADHA?:confused2::confused2:


kwenye muktadha wa baa, wakati mwingine inabidi tu kumwita kwa njia hii hasa wahudumu sugu wa baa za magomeni mapipa.....:confused2:
 
Nadhani wengi mmeshausikia huo mlio. Ni mlio ambao unatengenezwa kwa kukutanisha sehemu za juu na chini za mdomo (lips) na kuzifunga na hatimaye kuachia hewa iliyokusanyika kwa kuzifungua sehemu hizo kwa kutumia nguvu kidogo.
kweli hii fani inakufaa sana!
 
Naichukia sana hiyo style kwani ni ya kihuni,thru psss sikuwahi kugeuka kwani haina heshima wala nidhamu.Kwa sasa nadhani inatumika zaidi bar,,,lol
 
Mbona wauza maji na vocha kwenye mataa semu za magomeni ilala nyerere rod na chang'mbe wanabusubusu namnageuka kununua vocha au maji? hawa hwawauzi
 
Nadhani wengi mmeshausikia huo mlio. Ni mlio ambao unatengenezwa kwa kukutanisha sehemu za juu na chini za mdomo (lips) na kuzifunga na hatimaye kuachia hewa iliyokusanyika kwa kuzifungua sehemu hizo kwa kutumia nguvu kidogo. Matokeo yake ndio huo mlio.

Sasa nilipokuwa dogo, mtaani nilikuwa nikiwaona wakubwa zangu wakipiga huo mlio pindi waonapo mdada ambaye amewavutia akipita barabarani. Walikuwa wakifanya hivyo ili kuvuta nadhari yake kwao (draw her attention).

Kuna wadada ambao hawakupenda kusikia huo mlio na kuna ambao walipenda. Sasa mimi sielewi asili ya huo mlio nini. Halafu ningependa kujua kama siku hizi bado hiyo tabia ipo. Wadada wa humu yameshawahi kuwatokea hayo ya kupigiwa ppsss ppsss? Na kama yamewahi kutokea ulijisikiaje? Ulichukia? Ulifurahi?

Nakaribisha michango yenu...

Ahaaaa ngoja nicheke ila kwa sasa siyotena kwa madada imeshakuwa Honi!!au waulize makonda na wapiga debe ndo imekuwa njia rahisi yakuitia abiria!!au kwa Baiskeli isiyokuwa na Kengere utasikia psiiii!!ukisikia ukafikiri unaitwa pole! utasikia unapigwa taili!!!na kama ni kituo cha daladala ujue unaambiwa panda kwenye gari!!!! na kama hupo kariakoo shimoni!!,,,,mamayangu geuka haraka au kimbia lasivyo utatwishwa gunia la viazi!!:becky:
 
Back
Top Bottom