Powered by sasatel wengine mko wapi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Powered by sasatel wengine mko wapi

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Yona F. Maro, Oct 3, 2009.

 1. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #1
  Oct 3, 2009
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  POWERED BY SASATEL WENGINE MKO WAPI

  Wale ambao huwa wako maeneo ya mjini haswa jiji la dar es salaam lazima watakuwa wameona vibanda vya mawasiliano ya Internet ambavyo ni vya vodacom , eneo la mwenge kuliwahi kuwa na moja lakini kwa sasa limeshafungwa pale jijini dar es salaam kuna lingine liko Mtaa wa samora , Ukiingia ndani ya banda hilo kila siku mwendeshaji huwa na visingizio mara Mtandao uko down mara kuna virus vitu kama hivyo .

  Wengine ambao tulitembelea maonyesho ya sabasaba mwaka huu tuliojionea wenyewe jinsi kampuni hizi zilivyoweka huduma za mtandao kwenye mabanda yao kwa ajili ya watu mbali mbali kuweza kuwasiliana na wenzao wanapokuwa ndani ya uwanja huo .

  Nilibahatika kwenda kwenye banda la Tigo , Sasatel na Voda ila nilivutiwa zaidi na sasatel kwa sababu ndio ilikuwa iko sokoni kwa mara ya kwanza nilipenda kwenda kuona huduma zao Kulikuwa na huduma nzuri sema tatizo lilikuwa kwenye computer zao hazikuweza kukidhi mahitaji mengine ya watumiaji kama spidi , matatizo mengine kama virus kuna watu walikuwa wakiingia pale kutoka tu akienda nyumbani analia na virus , inaonyesha mtu aliyekuwa na wajibu wa kusimamia mambo yale pale hakuwa mwangalifu sana .

  Pamoja na yote hayo kwenye siku za karibuni nimejaribu kuangalia kama huduma zile za vibanda kule ndani zinasambazwa sehemu nyingi na kwa uzuri zaidi , nimegundua kwamba Sasatel wanasambaza huduma zile kwa kasi zaidi kuliko kampuni nyingine yoyote kwa kipindi cha miezi michache toka Wakati Ule .

  Nilivutiwa siku moja nilipopita sehemu nikakuta THIS INTERNET CAFÉ IS POWERED BY SASATEL , ikabidi niingie ndani kwenda kuona inakuwaje kwa zaidi ya masaa 5 hivi huduma zao zilikuwa nzuri , tatizo ni kama la hapo juu watu waliopewa kazi ya kusimamia internet café yenyewe ndio hawako vizuri katika mambo kadhaa .

  Huduma hizi za SASATEL nimevutiwa nazo sana wangefanya mkakati wa kuzipeleka sasa huko vijijini na sehemu ambazo kupatikana kwa huduma za mawasiliano ni kazi , kampuni nyingine zimeshindwa ila kwa mwendo huu wa SASATEL unaoonyeshwa sasa hivi naamini huko watafikia .

  Baada ya Wabunge kuendelea kupiga domo kuhusu huduma hizi ni wakati wao sasa kuongea na Kampuni kama hizi kwa ajili ya huduma za mtandao kwa wananchi wao haswa wale walio maeneo ya vijijini naamini wakiwa na mikataba maalumu kila mtu ataweza kufaidika na huduma hizi .

  Hata wananchi ambao wamejiunga kwenye vikundi vya saccos wanaweza pia kuongea na kampuni kama hizi kwa ajili ya kuletewa huduma katika maeneo yao , itasaidia wanachama wa saccos kuwasiliana na makao yao pia saccos itaweza kutengeneza faida zaidi kwa kulipisha watu

  Kama wananchi wanachanga pesa kwenye saccos kwanini wanashindwa kujipanga hivyo hivyo kupatiwa huduma za mawasiliano kama hizi huko vijijini mwao , Baada ya kuchangia Kwenye Vicoba .
   
 2. Amoeba

  Amoeba JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2009
  Joined: Aug 20, 2009
  Messages: 3,328
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 0
  Tunachotaka kuona hapa ni details za speed na bei. ni kipya gani walichonacho kitachonifanya nimhame ISP wangu wa sasa!....in details please, siyo sifa zisizo na support yoyote. wanaweza kuwa wazuri ila haujaeleza uzuri wao. karibu tena
   
 3. Ramthods

  Ramthods JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2009
  Joined: Jun 2, 2009
  Messages: 494
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  It would be better to quantify their qualities - not just expressing them!
   
 4. k

  khalids19 Senior Member

  #4
  Oct 6, 2009
  Joined: Jul 27, 2009
  Messages: 157
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  sasa we unataka nini?
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2009
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,344
  Likes Received: 3,111
  Trophy Points: 280
  kama hujalizika na huduma achana nayo....badala ya kulalamika saaaaaanaaaaaa.........
   
 6. B

  Bontowar JF-Expert Member

  #6
  May 15, 2010
  Joined: Feb 21, 2009
  Messages: 524
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  any update about sasatel
   
 7. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #7
  May 15, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  unavyosema huduma za kwenye banda la sasa tel unamaanisha huduma za customer service au hu duma za core communication service kama internet downlaodong na uploading speed na capacity?
   
 8. Tumsifu Samwel

  Tumsifu Samwel Verified User

  #8
  May 15, 2010
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 1,406
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 135
  Msidanganyike, Sasatel hawafai kabisa kwanza speed yao ni ndogo sana, na pia bei zao kwa MB ni kubwa sana unaweza weka 1000 elfu kabla ujafungua chochote ukashtukia imeisha..... Kwa yeyote anayetaka Modem yao (ile ya mezani) nitampatia bure!
   
Loading...