#Povertyporn, hashtag inayomtikisa Waziri

bukoba boy

JF-Expert Member
Joined
Jan 15, 2015
Posts
5,376
Reaction score
3,977
Wadau wanasema,vitendo vya watu kupiga picha/video wakisaidia wengine kisha kuzipakia mitandaoni,ni kama kutumia umasikini wa watu kwa faida binafsi.

Sasa watu wanahoji kama unatumia pesa za serikali,kufanya hivyo ni upumbavu sana.ni namna ya kujijenga kisiasa tu na wala sio "special moments",kwani hazimtokei waziri peke yake hata wao zinawatokea ila wanajitahidi kujizuia bila kuwepo na muafaka kati ya huyo aliyepigwa picha na anayetolea maelezo ya picha.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kuna jamaa alinichangia laki 6 kwenye harusi ya mwanangu lakini alikataa katakata kurekodiwa mchango wake popote. Alisema ile ni sadaka hata kamati wakikabodhiwa wasijulishwe nani katoa.

Makamba jifunze kwa mzee huyu.

Kwenye nyumba yetu ya ibara kulihitajika kufanya ukarabati wa paa kwa kuondoa mabati yote na kuweka mapya ya m south. Zilitakuwa kama bati 170 hivi, so tukawa waumini tunachangishana mdogo mdogo zikapatikana bati 100. Ghafla siku moja kiongozi wetu akatutangazia kwamba amegiwa simu na muumini mmoja ambaye hamjui kwamba aende kwenye hardware flani akachukue bati zote zilizobaki ,misumari , mbao na pesa ya ufundi. Ukarabati ukafanyika fasta na kukamilika. Mpaka leo huyo aliyetoa mchango wake mkubwa hakuwahi kujulikana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ni mbio za 2025 tu hizo zisikutishe sana,,
 
Unaona sasa!!! Sio makamba sahani ya wali tu picha kibao. Umaskini mbaya sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom