Postmortem Certificate ni kitanzi kwa serikali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Postmortem Certificate ni kitanzi kwa serikali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Luteni, Jan 13, 2011.

 1. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kama kweli serikali ilikubali kutoa hiyo hati na kama kweli Chadema au wafiwa wanayo hiyo hati mkononi na imeandikwa sababu ya kifo kuwa ni kwa kutobolewa na risasi, basi kwa kutumia hati hiyo serikali inaweza kushitakiwa kwenye mahakama yoyote ya kimataifa kama wahusika watataka kufanya hivyo.

  Kwa vile tukio lenyewe nila kisiasa zaidi na limehusisha watu wengi serikali inaweza kupata wakati mgumu kulimaliza kienyeji kwa mazungumzo labda tu kama wahusika(wafiwa) au Chadema au mashirika ya haki za binadamu yaamue kutolifuatilia.

  Nasema kwa serikali kukubali kutoa hati ya vifo vya maandamano ya Arusha imefanya kosa kubwa la mwaka ni kama imejifunga kitanzi yenyewe inasubiri huruma ya mvutaji.
   
 2. m

  mams JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 19, 2009
  Messages: 616
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  They can afford to pay.
   
 3. Maishamapya

  Maishamapya JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 1,280
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Hawakuwa na ujanja. Ndivyo RPC alivyosema ... "Walilazimika kutumia risasi za moto ... na watu wawili wamekufa."
   
 4. M

  Mkeshaji JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2011
  Joined: Jan 7, 2011
  Messages: 4,264
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mkuu mbona post sioni kama inatutaarifu kuwa hati hiyo imetolewa. Hebu tuweke sawa kido hapo, imetolewa au?
   
 5. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,937
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  How much is the cost of death?
   
 6. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2011
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  with ccm mindset=zero
   
 7. Quinine

  Quinine JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2011
  Joined: Jul 26, 2010
  Messages: 10,937
  Likes Received: 12,207
  Trophy Points: 280
  Serikali kushtakiwa Thursday, 13 January 2011 09:29 Na Waandishi Wetu, jijini Dar Leo

  FAMILIA za ndugu waliouawa kishujaa kwenye maandamano ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wameazimia kuishtaki Serikali kutokana na Polisi kusababisha vifo vya makusudi vya ndugu zao.Wakizungumza na Waandishi wa Habari baada ya mazishi hayo, wamesema wamesikitishwa na vifo vya ndugu zao kwa kuwa waliuawa bila hatia.

  Wamesema ndugu zao walipoteza maisha kutokana na polisi kutumia nguvu kubwa na kusababisha vifo vya watu hao na majeruhi kibao huku wengine wakikamatwa bila sababu za msingi.

  Kutokana na hali hiyo wameazimia kufungua kesi mahakamani kuishtaki Serikali kudai fidia kwa kupoteza ndugu zao ambao walikuwa tegemezi kwa familia zao.

  Familia za marehemu hao-Denis Shirima na Omary Ismail-zimeibuka na kuzungumzia azima hiyo kutokana na vifo hivyo vilivyotokea Januari 5, mwaka huu katika maandamano ya CHADEMA yaliyofanyika mkoani Arusha.

  Akizungumzia adhima hiyo, mwanafamilia mmoja ambaye hakutaka kuandikwa jina lake gazetini, amesema wamesikitishwa na vifo vya ndugu hao na hawapo tayari kuliachia suala hilo hewani hivyo ni lazima waiburuze Serikali mahakamani.
   
 8. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #8
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180

  Kesi yoyote inayofunguliwa kwa madai ya mauaji kwenye sheria au mahakama za kimataifa ( International Court of Justice or International Jurisdiction) haina option ya mtuhumiwa kufungwa ama kulipa faini. Yenyewe ina hukumu moja tu endapo it has been proved guilty, anafungwa kifungo jela kulingana na kuhusika au kushiriki kwake kwenye mauaji tajwa.

  Anyway kwakuwa CHADEMA wamependekeza kuundwa kwa Judicial Commission of Inquiry kuchunguza mauaji ya Arusha, tutahitaji kauli ya Mkwere kusikia anataka kusema nini. Hatutaki atuundie tume huyu Msanii wa kutupwa.
   
 9. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #9
  Jan 13, 2011
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 445
  Trophy Points: 180
  Luteni, Dr. Slaa has already made a good president, but the vote was stolen strategically by chakachua matokeos.
   
 10. Jackbauer

  Jackbauer JF-Expert Member

  #10
  Jan 13, 2011
  Joined: Oct 28, 2010
  Messages: 5,920
  Likes Received: 90
  Trophy Points: 145
  Mtu ni mali ya serikali(state'property),mtu yoyote anayekufa un-natural death inastahili shauri hili lifikishwe mahakamani na serikali.nionavyo polisi aliyehusika itabidi afikishwe mahakamani ili ijulikane kama alikuwa anatekeleza amri ya wakuu au alijiamulia mwenyewe.postmortem certificate inatakiwa ionyeshe kama ni kweli kabisa kabisa bila chembe ya utata kuwa risasi zilizowaingia zilisababisha vifo.tusubiri na kuona serikali ikijishtaki yenyewe!
  Kudai fidia itakuwa jambo la muhimu sana kwa ndugu wa marehemu kulifanyia kazi.
   
Loading...