MVUMBUZI
JF-Expert Member
- Jan 8, 2011
- 5,182
- 2,304
Siku za hivi karibuni katika posta ya Arusha (Meru na Clock Tower) kumekuwa na upotevu mkubwa wa vifurushi hususani vile vinavyotoka nje ya nchi. Hata pale ambapo kifurushi kina kuwa na tracking number lakini pindi tu kikifika Arusha kifurushi kinapotea katika mazingira ya utata.
Kuna wakati unakuta kikaratasi cha kuchukua mzigo kwenye sanduku lako lakini ukifika kaunta eti utaambiwa mzigo hauonekani na inaweza kuchukua hadi siku kadhaa za ufuatiliaji ndipo uambiwe ooh ulikuwa umechanganywa na hadithi nyiingi za kiujanja ujanja.
Tulichogundua ni kuwa kitengo cha sorting au kina wafanyakazi wasio waaminifu na hivyo kuiba vifurushi kwa njia za kijanja au wafanyakazi hao ni wazembe kupindukia na hivyo kutokuwepo umakini katika kufanya sorting.
Pia uchunguzi umeonyesha kuwako idadi kubwa ya wazee katika posta ya Arusha haswa Meru kiasi cha kushindwa kutimiza wajibu wao kwa ubora na umakini unaotakiwa.
Tunaomba mamlaka husika itusaidie kufuatilia jambo hili ili kuwabaini wafanyakai wasio waaminifu na wazembe na hivyo kusababisha upotevu mkubwa wa vifurushi ya wateja haswa ile vinavyotumwa toka nchi a Marekani na Ulaya.
Kwa mfano kwa kipindi cha mwaka mmoja nimepotea zaidi ya vifurushi vitano kwa maelezo eti anwani imekosewa wakati tangu mzigo unatumwa ninau track kwenye mtandao.