Post za Ualimu toka Wizara ya Elimu

Post za Ualimu toka Wizara ya Elimu

Naona tamko tu la Kawambwa kuwa kaajili walimu wapya lakini list ya walimu siioni. Lakini hata hivyo nawatakia utumishi mwema wa umma waajiriwa wapya.






TAARIFA KWA UMMA KUHUSU AJIRA YA WALIMU WAPYA WA SHULE ZA MSINGI, SEKONDARI NA VYUO VYA UALIMU TANZANIA BARA MWAKA 2012/13

Jumla ya walimu 26,537 wameajiriwa Serikalini kwa mwaka wa fedha 2012/13. Walimu wa ngazi ya cheti walioajiriwa ni 13,568. Kati yao walimu 13,527 wamepangwa kufanya kazi katika shule za msingi zilizopo kwenye Halmashauri na walimu 41 wamepangwa katika shule za msingi za mazoezi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Jumla ya walimu wa sekondari na vyuo vya ualimu walioajiriwa ni 12,973; wakiwemo walimu wa shahada 8,887 na wa stashahada 4,086.

Walimu waliopangwa kufundisha shule za sekondari zilizo chini ya Halmashauri ni 12,893, wakufunzi wa vyuo vya ualimu ni 59 na walimu 21 wamepangwa kufundisha katika shule za sekondari za mazoezi zilizo chini ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi. Aidha, idadi hiyo inajumuisha walimu 188 wa Elimu maalumu wenye Shahada ambao wamepangwa katika shule za sekondari na vyuo vya ualimu vinavyotoa Elimu maalumu.

Idadi ya walimu walioajiriwa mwaka 2012/13 imeongezeka kwa asilimia 11 sawa na walimu 2,630 ikilinganishwa na walimu 23,907 walioajiriwa mwaka uliopita 2011/12.

Kati ya walimu wa sekondari na vyuo waliyoajiriwa, jumla ya walimu 1,286 (shahada 862 na stashahada 424) ni wale walioomba ajira Serikalini kutoka soko la ajira. Hawa ni tofauti na wale waliotoka vyuoni moja kwa moja. Aidha, walimu walioajiriwa ni pamoja na walimu wa ngazi ya stashahada 841 wa mwaka 2011 waliorudia mtihani mwaka 2012 na kufaulu. Kwa upande wa walimu wa elimu ya msingi, walimu 200 kati ya walioajiriwa ni waliokuwa katika soko na kuomba ajira serikalini.

Naagiza kuwa walimu wahitimu ambao ni waajiriwa(inservice) wanatakiwa kurudi katika vituo vyao vya kazi walikokuwa wakifanya kazi kabla ya kwenda masomoni.

Orodha ya walimu na Halmashauri walikopangwa itapatikana kwenye tovuti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi (United Republic Of Tanzania - Ministry of Education and Vocational Training) na tovuti ya Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa–TAMISEMI (www.pmoralg.go.tz). Orodha hiyo pia itatumwa kwenye Mikoa na Halmashauri husika.

Walimu wote waliopangiwa vituo vya kazi wanaagizwa kuripoti katika Ofisi za Wakurugenzi wa Halmashauri au Wakuu wa Vyuo vya Ualimu walikopangwa tarehe 1 Machi, 2013. Tarehe ya mwisho ya kuripoti ni tarehe 9 Machi 2013. Tarehe ya mwisho ya kuripoti imepangwa ili kuwezesha walimu wapya kuingizwa katika orodha ya mshahara wa mwezi Machi 2013. Watendaji na wasimamizi wa elimu kwenye Halmashauri na Vyuo vya Ualimu watakuwepo kuwapokea.

Walimu wote wanatakiwa kuripoti wakiwa na Vyeti vyao halisi vya taaluma, cheti cha kuzaliwa, pamoja na nakala zake ili viweze kuhakikiwa na kukamilisha taratibu za ajira zao. Waajiri, yaani Wakurugenzi wa Halmashauri na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi watawalipa walimu wapya malipo stahili kwa mujibu wa nyaraka na miongozo ya Serikali kuhusu waajiriwa wapya.

Nawatakia walimu wote waliopata ajiri hizi mpya utumishi mwema Serikalini katika Sekta ya Elimu.​
Imetolewa na:​
Dkt. Shukuru Jumanne Kawambwa (Mb)
WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
13 Februari 2013
 
Mulugo anasema fedha ya kujikimu ni siku 7 tu na hela ya usafiri lakini hakuna hela ya mizigo maana hawa watu ni freshers from school hawana mizigo yeyote. Mbona freshers kwa kada nyingine wanapewa hela ya mizigo?
 
wameshaapload jamani sijui nifanyaje niweke hapa
 
haya ni majina ya walimu wa grade 3A ANGALIENI HAPA KAZI NJEMA MENGINE YANAFUATA
 
Subirini zipositiwa kwenye Web ya wizara tunajua mmesubiri sana lakini sasa imekuwa.
 
Ivi ungebakia kimya tu si bado ungeonekana wa maana kuliko kuweka kitu ambacho hakipo?
Sina uhakika hao walimu wanao ngoja ajira zao wakikuona watakwambia nini!!!
we hungojei? hahahahaha
 
acheni ujinga kama una uhaklika usidanganye watu wazima ni upumbafu acheni watu wana elimu zao za internet programming na wanashinda kwenye net sasa kwa nn udanganye idiot ww!
 
Mtakoma, mtasubiri sana, siku zote mnaouona ualimu mbaya, leo hii ajira zinatangazwa watu mna gombania keyboards za compute na wengine na visimu vya mchina......kazi kweli kwli....!!!
 
Post zipo kweli ila Web ya Wizara ya Elimu na Hata TAMISEMI zinazingua kufunguka kuna wakati nilibahatisha kufungua www.moe.go.tz nikaona wameziweka Post kwa chini kidogo upande wa kulia
 
mh! embu acha kuongea ovyo ww! ingekua uwalimu tunauzarau 2ngesomea 2yearz
 
jamani mbona kaweka link hapo?
 
Back
Top Bottom