Post yangu ya mwisho kuhusu elimu

zagarinojo

JF-Expert Member
Jul 26, 2020
2,622
2,835
Habari wana JF.
"Education is the key to success"
"Education for the bright future"

Hizi ni kaulimbiu za elimu tunazotumia hapa kwetu. Nina imani ufanisi wa elimu yetu unasadifiwa na hayo maneno..

Nina wasiwasi na mfumo wetu wa elimu.

Sidhani Kama unawaanda vya kutosha vijana wetu kuishi katika ulimwengu wa mabadiliko ya kisayansi na kiteknolojia.

Elimu yetu haina thamani ukilinganisha na elimu katika nchi za wenzetu.

Kwa mfano ukichukua msomi wa kwetu hapa mwenye degree moja ya Mechanical Engineering na mwingine wa ughaibuni aliye na degree moja ya Mechanical Engineering pia nafikiri utaona ni kiasi gani utofauti wa ubunifu,kufikiri na utendaji wa kitaaluma ulivyo mkubwa.

Je ni kwa sababu sisi hatuna akili?Loh!siamini katika hilo
Tatizo ninaloliona ni mfumo wa elimu yetu hautujengi kikamilifu.

Mfumo wetu wa elimu umejikita katika ufaulu wa marks na mitihani kuliko uelewa wetu

Siwezi kushangaa nikimuona mwanafunzi anacopy katika mitihani kwasababu mfumo wetu wa elimu umejikita katika ufaulu na sio uelewa.

Swali ambalo wanafunzi wengi huuliza ni kwamba "Mwalimu,je swai hili litakuwepo kwenye mtihani"

Mara ngapi walimu wametuchapa kwa kukosa notsi darasani lakini hawakuwahi kuhoji ufaulu wetu..!

Mfumo wetu wa elimu unawakaririsha wanafunzi mafacts Ili wajibu mtihani na wafaulu mwishowe uelewa wao unapimwa kwa mtihani tu...!

Nashindwa kuelewa ni kwanini tumekosa wasomi wabunifu na wenye kufanya mambo kwa vitendo badala yake tumebakia na wasomi wa nadharia na historia..

Endapo tungeandaliwa kuwa wabunifu na watu wa vitendo zaidi nahisi tungekuwa mbali..

Walimu wetu hutufundisha jinsi ya kufaulu na kujibu mitihani lakini hawatufundishi jinsi ya kuelewa maswali katika mitihani.

Walimu wanafundisha wanafunzi tofauti wenye ndoto tofauti,vipaji tofauti kwa njia moja tu na kitu kimoja.
Bila kuelewa kuwa kila mtu amepewa kipawa kwa nafasi yake.

Wapo wanaolewa kwa njia ya simulizi,wengine njia ya nyimbo,wengine kwa kujisomea wenyewe lakini wote watafundishwa kwa njia moja.

Je kuna umuhimu gani wa kuwatenga wanafunzi katika matabaka na madaraja mfano Slow Learners na Fast Learners
Unafikiri itakuwa njia sahihi ya wao kujifunza wakiwa katika hali hiyo.

Je hata walimu wetu tungewatenga katika matabaka na madaraja pia?
Hata mtaani pia tungejitenga pia walio na elimu wakae pekee yao na wasio na elimu pekee yao.

Nategemea kuona ukosoaji wenye kujenga na kuboresha mfumo wetu wa elimu kwa manufaa ya vizazi vijavyo
 
Back
Top Bottom