Posho ya Wabunge 200,000 ikipitishwa tufanyeje? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho ya Wabunge 200,000 ikipitishwa tufanyeje?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Petu Hapa, Jan 26, 2012.

 1. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #1
  Jan 26, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Sababu za kwanini posho isipandishwe zimeshasemwa sana na wananchi. Sijasikia sababu zozote za msingi, zinazojibu kwa kina hoja za wanachi juu ya ongezeko hilo. Lakini inawezekana kabisa Serikali kwa sababu zake ambazo inaona zinafaa, kwa kunguvu yake ya dola na kwa utambuzi kwamba watanzania wanakasumba ya kusema tu halafu mambo yanapita ikaamua kupitisha hili ongezeko la posho za wabunge.

  Sasa, Waziri Mkuu akiipandisha ama hata Raisi akirejea na kupandisha tufanye nini? Kama mwananchi Serikali ikifanya kitu ambacho sio kizuri na ninaona inakosea ama kuhatarisha amani na maendeleo ya nchi yake tunafanyaje? Tunaiambiaje serikali inakosea pale ambapo inaanza kujenga hulka ya kufanya tu mambo inavyopenda yenyewe bila kujali sauti za wananchi wake?
   
Loading...