Posho Tanapa zamkera JK

Saint Ivuga

JF-Expert Member
Aug 21, 2008
54,363
58,386
Posho Tanapa zamkera JK
Send to a friend
Sunday, 11 December 2011 21:24
0digg

enzi-hinzo.jpg
Rais Jakaya Kikwete akiangalia picha za baraza la serikali ya kwanza baada ya wakoloni kuondoaka wakati alipotembela maonyesho ya miaka 50 ya uhuru, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Jamson

Nora Damian na Geofrey Nyang’oro
RAIS Jakaya Kikwete ameitaka Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (Tanapa), kuacha kugawana posho badala yake, fedha wanazopata wazitumie kutangaza vivutio vya utalii vilivyopo nchini ili kukuza sekta hiyo.

Agizo hilo la Rais Kikwete limekuja kipindi ambacho nchi imekuwa ikitikiswa na mjadala wa posho mbalimbali serikalini na kwa wabunge ambazo tayari wasomi, wananchi na wanaharakati wanazipinga.

Akizindua Chuo cha Taifa cha Utalii Kampasi ya Dar es Salaam juzi usiku kilichojengwa kwa ushirikiano wa serikali na Ufaransa, Rais Kikwete alisema Tanzania ina sifa kubwa duniani ya kuwa na vivutio vya utalii, lakini idadi ya watalii wanaokuja nchini ni ndogo na haifikii hata milioni moja.

Alifafanua kwamba sababu kubwa inayofanya watalii wasije kwa wingi nchini, ni kutotangazwa kwa vivutio vya utalii vilivyoko sehemu mbalimbali nchini.

“Tanapa mnazo hela nyingi, nyingine mnatumia kugawana posho tu na wengine kama Ngorongoro wanaongeza safari za wajumbe wa bodi tu kuzunguka dunia nzima,”alisema Kikwete na kuongeza kuwa:

“Acheni kulalamika, tangazeni vivutio vya utalii hamuwezi kushindwa na msitangaze Marekani tu, tangazeni pia utalii wetu nchini Ufaransa, Japan na kwingineko,”alisema.

Alisema utalii unachangia asilimia 17.2 ya pato la taifa na unaongoza kwa kuiletea nchi pesa za kigeni na kwamba ni miongoni mwa sekta zinazoajiri watu wengi zaidi nchini.

Rais Kikwete pia alikitaka chuo hicho kuhakikisha kinatoa wahitimu wazuri ili kuondoa malalamiko yaliyopo na kwamba kazi nyingi za sekta hiyo, zinachukuliwa na wageni.

Alisema katika baadhi ya hoteli hapa nchini, wageni wako wengi kwa sababu Watanzania walio wengi ni wa viwango vya chini.

“Wakati mwingine najisikia mnyonge kila ninapokwenda nakuta majirani zetu wapo, lakini Watanzania hawapo. Hatufikii viwango, kazi yetu ni kulalamika tu na kama hatutabadilika tutapata taabu sana, wageni watazidi kuajiriwa,”alisema.

Chuo hicho kimejengwa kwa gharama ya Euro 7,725,529 (Sh 17,768,716,700) ambazo kati yake Euro 1,955,152 (Sh 4,496,849,600) zimetolewa na serikali ya Tanzania na nyingine zimetolewa na serikali ya Ufaransa kupitia Shirika lake la Maendeleo (AFP).

Chuo hicho chenye hadhi ya kimataifa kina uwezo wa kuchukua wanafunzi 500 kwa wakati mmoja. Kina maabara ya chakula yenye vifaa vya kisasa, mgahawa, ukumbi wa mkutano na sehemu ya mafunzo kwa vitendo.

Septemba mwaka huu Rais Kikwete aliapa ataanza kuchukua hatua kwa watendaji wakuu wa Serikali na wadau wa sekta ya ujenzi wenye tabia ya kuomba na kupokea rushwa wakati wa mchakato wa zabuni ili iwe fundisho kwa wengine wenye tabia kama hiyo.
Akifungua mkutano wa wadau wa sekta ya ujenzi Dar es Salaam alisema sekta hiyo nayo inanuka rushwa kutokana na baadhi yao kutoa fedha ili kupata kandarasi.

Zitto azungumzia posho
Wakati huohuo, Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Kabwe, naye ameonya kuwa kitendo cha wabunge kujilimbikizia posho, kinajenga hali ya kutoaminika mbele ya jamii wanayoitumikia.

Akizungumza kwenye harambee ya mavuno iliyoandaliwa na Kanisa la Anglikana la Mtakatifu Nikolao na Mashihidi wa Afrika, Ilala Dayosisi ya Dar es Salaam, Zitto alisema, wabunge ni wawawilikishi wa wananchi hivyo kitendo chao cha kujilimbikizia posho, kinajenga hali ya kutoaminika miongoni mwa jamii.

“Hivi sasa kuna hali ya kutoaminiana miongoni mwa jamii ya Watanzania na hili linasababishwa na sisi wenyewe viongozi. Ninyi mmetuchagua twende Dodoma tukawafanyie kazi ya uwakilishi ili maisha yenu yaweze kuwa bora, lakini hili la posho linafanya pasiwe na hali ya kuaminiana sababu mtaona kazi yetu ni kujilimbikizia mali badala ya kuwawakilisha,”alisema Kabwe.

Kabwe alirudia wito wake kwa Rais Jakaya Kikwete kutosaini sheria ya ongezeko la posho za wabunge na kuwataka wabunge wote waliokwishapokea posho hizo kinyume na utaratibu wazirudishe.

“Nimesikia rais hajasaini sheria ya ongezeko la posho. Ninamuomba asisaini na wabunge waliokwishalipwa fedha hizo kinyume na sheria kabla ya kusainiwa kwa sheria hiyo, wazirejeshe,”alisema.

Zitto alitumia fursa hiyo kuwaomba viongozi wa dini kukemea nyongeza ya posho za wabunge kwa uwazi na kuwaombea ili waweze kuwa waadilifu zaidi.
 
Wanaongezeana SAFARI ZA KUZUNGUKA DUNIA NZIMA mmhh kaazi kweli kweli.
 
This guy never stop to amaze me! Rais mzima "unakerwa" tu? Hakuna la zaidi. Halafu kuna miafrika humu inataka tumpigie makofi!! @#$%^&*()__+*&&&&&$%^&*() zao.
 
- Ila kwa kweli hawa watu huwa wana spend mno. TANAPA NA NGORONGORO, mfano mwaka huu tu mhifadhi mkuu wa mamulaka ya hifadhi ya ngorongoro alitumia BILIONI 8 kusafili nje ya nchi, huyo ni Mhifadhi mkuu peke yake katumia bilion 8 je hao wengine
 
Toba!!!!!!!!!!!!!!!!!!!! afu bado wanuza na Twiga wetu?hawa jamaa hawatosheki,jamaa anamijihela kumbe posho na mgao wamauzo ya twiga
 
Jk,uko right,ni bora hata wangeongezewa wabunge maana wanafanya kazi kubwa sana,kuwakilisha wananchi si kazi ndogo jamani
 
Back
Top Bottom