Posho, kivuko vyaiweka CCM njia panda | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho, kivuko vyaiweka CCM njia panda

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 7, 2012.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  SUMAYE AMVUTIA PUMZI NDUGAI
  Waandishi Wetu
  Mwananchi

  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimebaki njia panda baada ya kushindwa kuchukua hatua au kutoa tamko kuhusu mivutano na vita ya maneno inayoendelea sasa baina ya makada wake kuhusu masuala mawili makubwa yanayoigusa jamii.Masuala hayo ni nyongeza ya posho kwa wabunge ambayo imewaingiza katika vita ya maneno, Waziri Mkuu mstaafu, Frederick Sumaye na Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai.

  Suala jingine ni lile linalohusu ongezeko la nauli katika Kivuko cha Kigamboni ambalo limezusha malumbano baina ya Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli na wabunge wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiongozwa na wale wa CCM.
  Jana, CCM Taifa kupitia kwa Katibu wake wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye kimetaka kisihusishwe katika misuguano hiyo ya posho na nauli za kivuko kwa sababu hoja zinazojadiliwa si za kiitikadi.

  Wakati CCM Taifa ikisema hayo, chama hicho Mkoa wa Dar es Salaam, kupitia Kamati ya Siasa, kimetoa tamko la kumtaka Dk Magufuli aombe radhi kutokana na msimamo wake mkali wa kutetea kupanda kwa nauli.

  CCM Dar es Salaam wamekwenda mbali zaidi pale Mwenyekiti wake, John Guninita iliposema kuwa tayari wamefanya mawasiliano na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda na kukubaliana naye kwamba suala hilo linaweza kupatiwa suluhu.
  "Nimeongea na Waziri Mkuu (Mizengo Pinda) mambo haya yanazungumzika nawataka tu wananchi wawe na subira kwa wakati huu," alisema.

  Huku CCM mkoa ikitoa msimamo huo, wabunge wa Dar es Salaam wamepanga kukutana tena leo kujadili hatua za kumchukulia Dk Magufuli wakidai makali ya kupanda kwa nauli za kivuko tayari yamejitokeza kwa bei ya bidhaa eneo la Kigamboni kuongezeka.

  Kwa upande mwingine, Sumaye ametoa msimamo wake jana kwamba anamvutia pumzi Ndugai juu ya hoja zake alizotoa kuwa yeye (Sumaye) hana usafi wa kupinga ongezeko la posho za wabunge.

  Hali hiyo tete inakifanya chama hicho tawala kujikuta kikiwa na kauli zinazojichanganya kuhusu msuguano unaoendelea kama ni kukua kwa demokrasia au ni utovu wa nidhamu wa kutozingatia kupingana kupitia vikao vya chama.

  Kauli ya Nape
  Nape alisema jana kuwa kukitaka chama hicho kutoa kauli juu ya hoja zinazobishaniwa ni kutokitendea haki. Alisema hoja hizo ni za msingi na haziwahusu tu wabunge wa CCM, bali hata wa vyama vya upinzani. "Haya ni mambo ya msingi msiyatafutie itikadi."

  Alisema katika suala la posho, wapo wabunge wa Chadema wanaounga mkono na wanaopinga na vivyo hivyo kwa CCM.
  Alitoa mfano akisema yeye alipinga posho kwa wabunge sawia na msimamo uliotolewa na viongozi wa Chadema ingawa ndani kulikuwa na wabunge wanaoupinga hoja ya uongozi huo.

  Kuhusu suala la vivuko, Nape alisema wabunge waliotoa msimamo, ndani yake yumo wa Chadema, John Mnyika: "Hivyo katika suala hili chama hakipo."

  CCM Dar
  Wakati Nape akisema hayo, CCM Mkoa wa Dar es Salaam walikuwa kwenye mkutano na waandishi wa habari kutoa msimamo kuhusiana na mvutano uliopo baina ya wabunge wake, wengi wao wakiwa ni wa CCM na Dk Magufuli.

  Katika mkutano huo, Guninita alimtaka Dk Magufuli awaombe radhi wakazi wa Kigamboni kwa kauli yake aliyotoa hivi karibuni kuwa wanaopinga kupanda kwa gharama za kivuko; wapige mbizi wakati wa kuvuka bahari badala ya kutumia kivuko.

  Guninita alisema kauli hiyo imejaa dharau, kejeli na siyo ya kiungwana... "Chama kimepokea kwa masikitiko makubwa juu ya kauli zilizotolewa na Mheshimiwa Magufuli kwa wananchi wa Dar es Salaam, hususan wakazi wa Kigamboni kuwa kama hawawezi kulipa nauli mpya basi wapige mbizi."

  Pia alilaani kauli ya Dk Magufuli dhidi ya Mbunge wa Kigamboni (CCM), Dk Faustine Ndungulile kuwa kama anawaonea huruma wananchi wanaotumia kivuko hicho basi anunue boti itakayoitwa "kwa jina lake au la chama chake."
  Alisema: "Kauli kama hiyo haijengi mshikamano na ushirikiano kati ya uongozi wa CCM na Serikali. Hata kama malalamiko ya wananchi hao hawezi kuyasikia … asingetumia maneno hayo."
  Kwa sababu hiyo wakamshauri; "Tunamtaka awe kiongozi aliye tayari kushirikiana na kushauriana na viongozi na wananchi wakati wa kutekeleza Ilani ya CCM, jambo ambalo haliwezi kuathiri katiba na kanuni za taratibu za majukumu ya wizara na nchi kwa ujumla."

  Guninita ambaye alikuwa akizungumzia ripoti ya kikao cha Kamati ya Siasa ya Halmashauri ya CCM Mkoa wa Dar es Salaam iliyokaa juzi, alisema wanaungana na wabunge wa mkoa huo kuwa mabadiliko yaliyofanywa ni makubwa.
  "Hebu ona Guta ambalo ndicho chombo kinachoendeshwa na mlalahoi kabisa linapandishwa nauli kutoka Sh200 hadi Sh1,800! Haya ni mabadiliko makubwa," alisema.

  Sumaye
  Jana Sumaye alisema anajipanga kumjibu Ndugai juu ya hoja zake alizotoa kuwa, kiongozi huyo mstaafu wa shughuli za Serikali hana usafi wa kupinga kuongezwa kwa posho za wabunge. Alisema yupo safarini kurejea Dar es Salaam na akifika ndipo atakapojua ni jinsi gani atakavyomjibu Ndugai.

  Akizungumza katika kipindi cha dakika 45 kilichorushwa na Kituo cha Televisheni cha ITV, Januari 3, mwaka huu Sumaye alisema hatua ya Bunge kujipandishia posho ya kikao kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku haiingii akilini na kwamba inakiuka utaratibu uliowekwa na Serikali katika kulipa gharama kwa maofisa wake.

  Kauli hiyo ndiyo iliamsha hasira za Ndugai ambaye alisema Sumaye hana uadilifu wa kuzungumzia posho za wabunge kwani akiwa Waziri Mkuu, alifanikisha kupitishwa sheria ya malipo kwa viongozi wakuu wastaafu ili kujinufaisha.

  "Kwa sasa analipwa asilimia 80 ya mshahara wa Waziri Mkuu aliyepo madarakani. Ni fedha nyingi kuliko hata mshahara wa Naibu Spika (Ndugai kwa sasa), wakati sheria hii inapitishwa alikuwa kiongozi wa shughuli za Serikali bungeni (Waziri Mkuu), alikuwa anajiandalia mazingira ya kustaafu," alisema Ndugai.

  Habari hii imeandaliwa na Leon Bahati, Zacharia Osanga na Fredy Azzah.
   
 2. Tony Almeda

  Tony Almeda JF-Expert Member

  #2
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 397
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mh! Vita vya panzi.......................!
   
 3. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #3
  Jan 7, 2012
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Seriously wanategemea Magufuli aombe radhi!! By the way Pinda akiamua kuzuia maamuzi yake ya hivi sasa tutaona movie nzuri sana. Itakuwa mara ya pili kwenye kipindi hichi and I dont think the Dr will take it lightly.... Who will brink first?
   
 4. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #4
  Jan 7, 2012
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,609
  Likes Received: 82,182
  Trophy Points: 280
  ...Wacha waparurane ili wazidi kukidhoofisha chama chao cha Mafisadi/magamba.
   
 5. Consigliere

  Consigliere JF-Expert Member

  #5
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 8,047
  Likes Received: 7,507
  Trophy Points: 280
  Wanategemea Pinda aingilie utendaji wa Magufuli? Akithubutu kufanya hivyo nina uhakika Magufuli atastaafu na safari hii hawataweza kumsihi kama walivyofanya wakati ule.
  Pili hao wabunge wanafahamu nini kuhusu heshima au dharau, vipi kuhusu kauli za huyo Guninita alipomshambulia Sitta mwaka jana na hata alipokuwa speaker, wakati yeye Guninita akitetea mafisadi? Je kwa kutetea kwake hao mafisadi haikuwa dharau kwa wananchi?
  Acha waendelee kujicholesha na kujiandalia the great fall, we are watching.
   
 6. ndogwila

  ndogwila Member

  #6
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 10, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 5
  nafikiri itakuwa ngumu sana dr. kuomba radhi kwa jinsi ninavyomfahamu,issue ya bwana Job na Sumaye inaandaa mazingizira mazuri ya kufanya mabadilko kwani siku fred akijibu tutapata mengi zaid na hizi zote ni rasilimali nzuri za kuingia nazo uchaguzi 2015,tujitahidi tusisahau tu,they're digging their own grave.
   
 7. ntamaholo

  ntamaholo JF-Expert Member

  #7
  Jan 7, 2012
  Joined: Aug 30, 2011
  Messages: 10,144
  Likes Received: 2,104
  Trophy Points: 280
  wewe pekee ndo wayakumbuka hayo, wengine tusha sahau, c wajua siye wazee wa matukio? tukio moja likitoka linashika kasi, likiibuka lingine, la kwanza tunapotezea tunaambatana na lingine. ingizo jipya
   
 8. P

  Paul J Senior Member

  #8
  Jan 7, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 193
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi kweli hawa ndo viongozi tulionao wanaojidai kuwa wanawatetea walalahoi? Huu ni unafiki mtupu. Nasema ni unafiki kwa sababu kupandishwa kwa nauri ya kivuko MV Magogoni na Kigamboni halina tofauti na mfumuko wa bei tunaoushudia kwenye bidhaa nyingine za muhimu katika maisha ya kawaida ya walalahoi! Haingilii akilini watu wazima wanakomalia kupanda nauli ya kivuko huku wakifumbia macho kupanda kwa gharama za maisha kwa vitu vingine na waseme eti wanamuonea mlalahoi. Huu ni unafiki wa viongozi vipofu! Kama kweli muyasemayo yatoka mioyoni mwenu basi pinga mfumuko wa bei ambapo kwa sasa kg1 ya maharage imefikia Tsh 2000 na mchele 2500 hapo Dar. Acheni unafiki na kutafuta political popularity kwa mambo yasiyokuwa ya msingi!
   
 9. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #9
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Jamani mimi nashanga unafiki wa viongozi wa chama cha magamba kujifanya kutetea wananchi wakati serikali ya iko hoi bin taabani kimapato. viongozia wa CCM wa siku hizi hawana maadili ya kiuongozi. kuwa chama tawala haina kutawala utendaji wa serikali.

  Nakumbuka mwaka 1998 baada ya elnino nikiwa pale Dodoma, Halmashauri zote ukusanyiji wao wa mapato ulikuwa chini sana kwasababu watu hawakuwa na kitu mvua ilisomba mazao yao. Lakini katibu wa CCM wakati huo Mr mzuri aliwaambia watendaji kuwa lazima wakusanye kodi kama mtu hana kamata kuku, mifungo na chochote alichona mtu. Na wananchi wakilalamika wao (ccm) watawalainisha kwani wao ni grisi. Alisema hivi akijua kuwa bila serikali kupata fedha hata chma hakitapata ruzuku. Wao ccm ndo wanachukua ruzuku kubwa, fedha hizo ni makusanyo kutoka vyanzo mbalimbali kikiwemo na kivuko cha kigamboni.

  Sasa nashangaa unafiki wa viongozi wa CCM wa siku hizi, hawana lolote zaidi ya kutafuta cheap populality kwa wananchi. Nami nasema Dr hawezi kuomba msamaha.
   
 10. P

  P.R.O Member

  #10
  Jan 7, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani, viongozi we2 cjui wanatupeleka wapi,huyu Magufuli mbona amebadilika ghafla?..nchi yetu inapotea,.me nilitegemea Magufuli aje kuwa Raisi baadae bt m wrong
   
 11. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #11
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  ccm nimependa msimamo wenu kwani suala la kivuko lilianza kufanywa la ccm yote wakati ni la wizara ya ujenzi. good show!!!!!!!!!!
   
 12. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #12
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kama magufuli ni kiongozi msikivu amesikia kauli za chama chake CCM kwamba ongezeko katika Guta, Bajaj, magari,baiskeli na pikipiki ni kubwa. mimi naona nauli ya sh. 200 si tatizo sana linaweza kujengewa hoja na wakazi wa kigamboni wakaelewa.
   
 13. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #13
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  kauli za CCM na serikali ni muhimu ni kuimaisha demokrasia si kuparurana, ukomavu wa kisiasa ni pamoja na kutoa uhuru wa maoni na kujieleza. CCM wangekaa kimya pia tungesema....why?
   
 14. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #14
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  .

  Na wewe tuombe radhi wanaJf kwa maneno yako haya ukikataa hautakuwa tofauti na pombe magufuli
   
 15. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #15
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  .

  kila jambo lina mwanzo kwani haba na haba hujaza kibaba mbeba yote kwa pupa hulikologa. mimi naona huu ni mwanzo mzuri tukianzia hapo na kufanikiwa tutaweza kushughulikia pia maeneo mengine. kufanya kosa si kosa ila kurudia kosa .....makosa ya nyuma yasitufanye kufumbia macho makosa mapya
   
 16. M

  Molemo JF-Expert Member

  #16
  Jan 7, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  Magufuli a.k.a Augustine Mrema amekabwa koo sasa
   
 17. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #17
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  Ndugai ni mmoja wa waliopitisha maslahi ya viongozi wastaafu ikiwemo nafasi ya waziri mkuu kwa nini hakupinga bungeni wakati wa kujadili muswada huo. kwani mtanzania akiwemo Sumaye akitaka kugombea Urais ndio aogope kusema? makosa aliyofanya Sumaye hayamzuii kujikosoa hata kama aliyafanya yeye.uongozi bora unaanza na hatua ya kujikosoa hata kama alihusika kupandisha posho za wabunge wakati wa kipindi chake. Sumaye anasema wabunge mnampa wakati mgumu Rais kikwete kwa kujiongezea maslahi bila kujali hali ya kipato cha watanzania walio wengi....kosa liko wapi. wabunge ni wabinafsi na kwa kweli mnampa Jk wakati mgumu
   
 18. Mkondakaiye

  Mkondakaiye JF-Expert Member

  #18
  Jan 7, 2012
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 839
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kwani nanyi wanaJf ni wanafiki kama viongozi wa ccm?
   
 19. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #19
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  wapo wanafiki hapa ambao wanaleta siasa kwenye mambo ya kiuchumi. Tunazungumzia hali ya kipato na uchumi wa wakazi wa kigamboni na kupanda kwa gharama za kivuko wao wanaleta UCCM na Uchadema hapa. Watuombe radhi
   
 20. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #20
  Jan 7, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  magufuli a.k.a Godbless Lema amekabwa koo sasa
   
Loading...