Posho haiwezi kunitemesha ubunge-Mrema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Posho haiwezi kunitemesha ubunge-Mrema

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 29, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 29, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,604
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustino Mrema  Mbunge wa Vunjo (TLP), Augustino Mrema, amewaponda wabunge wanaotaka kujiuzulu ubunge kutokana na posho kuwa ndogo, kwa kuwaeleza kwamba wasitawaliwe na tamaa ya fedha kwa sababu ubunge hauhitaji mpaka uwe

  milionea ndipo uweze kuwatumikia wananchi waliokuchagua.
  Mrema alisema hawezi kujiuzulu ubunge eti kwa sababu posho ni ndogo bungeni kwani wananchi walimchagua ili

  awatumikie kuwaletea maendeleo na siyo kwenda kufuata posho.
  “Mimi siachii ngazi ng’o, fedha siyo ishu kwangu nawatahadharisha tunaolipwa posho na malupulupu tusitawaliwe na tama ya fedha wananchi wanatuamini hivyo tuwatumikie,” alisema Mrema.

  Mrema alisema ni kweli posho ni ndogo kwa wabunge, lakini hata hizo kidogo zinazotolewa inategemeana na huyo anayepewa anazitumia vipi maana ukizidisha matanuzi haziwezi kutosha na siku zote fedha huwa hazitoshi hata kama

  kila mbunge angelipwa posho ya Sh. milioni 10.
  Mrema aliongeza kuwa kauli ya Spika wa Bunge, Anne Makinda, kwamba kuna wabunge wanataka kujiuzulu ubunge kwa sababu posho ni ndogo, hayo ni maoni yake.
  CHANZO: NIPASHE
   
Loading...