Porokwa akacha kumvaa Lowassa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Porokwa akacha kumvaa Lowassa

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Jun 7, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Jun 7, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,607
  Likes Received: 4,599
  Trophy Points: 280
  NA SULEIMAN JONGO

  KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), mkoani Arusha, Daniel ole Porokwa, aliyetangaza nia ya kuwania ubunge Monduli katika uchaguzi mkuu wa Oktoba, mwaka huu, amejiondoa kwenye kinyang'anyiro hicho. Akizungumza na waandishi wa habari mjini Dar es Salaam jana, Porokwa alisema amefikia uamuzi huo baada ya kushauriwa na wazee.

  Kwa mujibu wa Porokwa, wazee wamemshauri asipambane na mbunge wa sasa wa jimbo hilo, Edward Lowassa, ambaye pia aliwahi kuwa Waziri Mkuu, kwa kuwa ni kiongozi mkuu wa kimila. Porokwa alisema baada ya kutangaza nia ya kuwania ubunge katika jimbo hilo, alikwenda jimboni kuona jinsi wapiga kura walivyopokea kauli yake, ndipo alipopata maombi ya kumtaka asubiri.

  Alisema akiwa katika ziara hiyo, alifuatwa na viongozi wa kimila wa Kimasai, ambao walimshauri asitishe uamuzi wa kugombea ubunge katika jimbo hilo kwa sasa na kumpa Lowassa nafasi ya kumalizia miaka mitano ijayo.


  "Baada ya kuutafakari kwa kina ushauri huo ambao nilipewa na viongozi wa kimila na kushauriana na familia na marafiki zangu, nimeamua kwa moyo mweupe kusitisha uamuzi wa kugombea," alisema Porokwa.

  Alisema pia alifikia uamuzi huo baada ya kutambua ukweli kwamba, Lowassa ndiye kiongozi mkuu wa kimila wa wazee wa Kimasai (Malaigwanani), hivyo kupambana naye ni kitendo kisichofaa.

  Porokwa alisema licha ya kutumia haki yake ya kikatiba kutangaza nia, ni ukweli usiopingika kuwa, chini ya Lowassa jimbo hilo limepiga hatua kimaendeleo na kwamba, safari hii ndiyo itakuwa ngwe yake ya mwisho.

  "Natambua yatasemwa mengi kutokana na kujiengua, kwani hata nilipotangaza nia wapo waliosema nimefanya hivyo kwa kutumwa na wapinzani wa Lowassa kisiasa. Nimefanya hivyo bila shinikizo la mtu yeyote," alisema.


  Porokwa akacha kumvaa Lowassa
   
 2. telele

  telele Member

  #2
  Jun 7, 2010
  Joined: Jun 4, 2010
  Messages: 29
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  pole porokwa! hatimae umejiingiza mtegoni kama ambavyo tulitegemea itakuwa hivyo siku tuliposikia umetangaza nia ya kumpinga lowasa. ambalo hatuna uhakika nalo ni kwa dau la shilingi ngapi umenunulika, au ahadi tuu zimekulaghai kama ambavyo tunamjua edward nae alivyo mzee wa ahadi nyingi kama mzee wa bagamoyo alivyo. kiufupi umejidhalilisha.

  lowasa siyo mmasai ni mmeru na hicho cheo unachompa alishavuliwa baada ya ukweli kubainika kwamba siyo mmasai. lowasa baba yake ni mmeru na mama yake ndio mmasai kwa mila za kimasai huwezi kufuata ukoo wa mama hata siku mmoja. wazee wa kimasai walipobaini kuwa jamaa aliwadanganya na kujipachika umasai hadi akapenya kuwa mbunge wao wakamvua u Laigwanani. mmeru hawezi kuwa laigwanani wa wamasai
   
 3. Kisoda2

  Kisoda2 JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2010
  Joined: May 30, 2008
  Messages: 1,240
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kaazzzzzzzzzz kweyi kweyiiiii
   
 4. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #4
  Jun 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hicho ni kipima joto cha siasa jamani.

  Ametumwa kutoa ujumbe kuwa EDO bado anataka kugombea na kuwaandaa wazee ili waonyeshe kuwa bado ni chaguo lao. Kwa mantiki hiyo atakuwa ni mgombea wa SSM asiye na upinzani toka SSM? Sasa wapinzani jiandaeni na ilani inayouzika kwa kuwa sasa itakuwa ni salama kumdondosha huyu fisadi. Du kweli siasa ni fumbo!
   
 5. M

  Mchili JF-Expert Member

  #5
  Jun 7, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 727
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kashalamba michuzi huyo, na ndio ilikuwa lengo lake
   
 6. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #6
  Jun 7, 2010
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Huyu Porokwa analifahamu hili mkuu?

  Kama halijui hili basi kwa wale watu wake wa karibu wanaotembelea hapa wampe taarifa hii ili na wengine waweze kuitumia kwa kuibua kwa wazi kuwa EDO si mkweli ni mwongo na fisadi wa kutupa hadi amelihadhaa kabila la kimasai kwa kuwadanganya kuwa ni mmasai. Piga chini huyo! Abakie kula mihela ya richmond na ile ya mashamba (ni setler mkubwa sana huyu) na mtu wa real estate nyinginezo maana aliiba na akawekeza vilivyo. Hana aibu.

  Nikikumbuka alivyoitumia Wizara ya Ardhi ... kikamilifu kujipatia viwanja na mashamba!!! Kila mahali likiwekwa linawaza namna ya kukwapua tu, jizi hili.
   
 7. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #7
  Jun 7, 2010
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,632
  Trophy Points: 280
  Wanasiasa wa aina ya Parokwa wamejaa sana katika siasa za Tanzania,na hii ni sababu kubwa kwanini nchi yetu kamwe haiwezi kupiga hatua za kimaendeleo pamoja na kuwa na rasilimali nyingi na za kutosha.Tangu alipotangaza nia ya kugombea nilijua hatoweza kusimamia kauli yake sana sana nilijua njaa zilikuwa zinamsumbua.
   
 8. Bill

  Bill JF-Expert Member

  #8
  Jun 7, 2010
  Joined: Oct 5, 2007
  Messages: 4,145
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Nina jamaa yangu anataka kutia timu ili kutafuta fedha tu kwani anatambua jamaa atamshikisha ili ajitoe kisha amuunge mkono. Nachelea kuamini ndiyo njia aliyoitumia Porokwa ili japo kutunisha mfuko wake kwa siku mbili ama tatu hivi.:A S-confused1:
   
Loading...