Pdidy
Platinum Member
- Nov 22, 2007
- 61,802
- 38,012
Kashfa ya Richmond: Ikulu yasema mapendekezo ya Bunge lazima kufanyiwa kazi
Na Ramadhan Semtawa
BAADA ya mkutano wa 17 wa Bunge la Muungano kushindwa kujadili ripoti ya utekelezaji wa hatua dhidi ya kashfa ya Richmond, Ikulu jana imesema kuwa bado suala hilo liko mikononi mwa muhimili huo wa nchi na kwamba wananchi wasubiri maamuzi.
Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo aliwaambia waandishi wa habari jana kwamba, kashfa ya mkataba wa kifisadi kati ya kampuni hiyo ya Richmond Development (LLC) na Tanesco, iko mikononi mwa Bunge, ambalo limekuwa likipiga kelele bila mafanikio kutaka hatua zichukuliwe dhidi ya wahusika wote waliotajwa kwenye ripoti ya kamati teule.
Luhanjo, ambaye ni mkuu wa mamlaka ya nidhamu anayetakiwa kuchukua hatua kwa baadhi ya watumishi waliotajwa katika kashfa hiyo, ametoa kauli hiyo wakati hadi sasa kuna watendaji ambao hawajawajibishwa na Ikulu, akiwemo Mkurugenzi wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Dk Edward Hoseah.
Akijibu swali la gazeti hili jana, Luhanjo alisema Ikulu haiwezi kuingilia bunge.
"Najua wewe umechomekea tu hilo swali, ni kazi yako kuchomekea... suala la Richmond sasa hivi liko mikononi mwa bunge, sasa si vema kuanza kuingilia kwa undani mambo ambayo tayari yako bungeni. Tuache bunge liendelee na kazi yake na kufanya maamuzi," alisema Luhanjo.
Luhanjo alisema serikali katika kusimamia maadili ya utumishi wa umma ina vyombo vyake kwa ajili ya kulinda maadili ya sekta hiyo.
"Tunavyo vyombo muhimu vya kuangalia maadili ya utumishi wa umma kuanzia hapa Ikulu, vipo vyombo na serikali iko makini katika hilo," alifafanua Luhanjo.
Kwa mujibu wa Luhanjo, katika mambo yanayohusu maadili ya Utumishi wa Umma, serikali imekuwa ikitumia vyombo vyake kuhakikisha yanalindwa na kuzingatiwa.
Alisema si kweli kwamba hakuna mkazo katika kusimamia maadili ya Utumishi wa Umma.
Mkutano wa 17 wa bunge, ulimazika huku suala la Richmond likionekana kupigwa danadana kwa mwaka mzima sasa tangu bunge litoe maazimio 23 Februari mwaka jana na kuipa serikali miezi sita kuyatekeleza.
Awali serikali, ikionekana kuliburuza bunge, iliahidi kuwa ingewasilisha ripoti ya utekelezaji wa maazimio hayo kwenye mkutano wa Kamati ya Nishati na Madini, lakini baadaye ikatangaza kuwa imekubaliana na kamati hiyo kuwa ripoti ipelekwe moja kwa moja Dodoma.
Hata hivyo, suala hilo halikuwekwa kwenye ratiba ya shughuli za mkutano wa bunge na badala yake likapigwa danadana hadi ilipotangazwa kuwa halitajadiliwa tena.
Kashfa ya Richmond ambayo iliibuka katika mkutano wa 10 wa Bunge, ilihusu utoaji wa zabuni ya uzalishaji wa umeme wa dharura bila ya kufuata taratibu na kuipa mkataba Richmond ambayo ilibainika kuwa haikuwa na uwezo.
Kashfa hiyo ilisababisha Edward Lowassa kujiuzulu wadhifa wake wa waziri mkuu baada ya kutakiwa na kamati teule ya bunge kutumia busara zake kutokana na kutajwa sana na vyombo vya habari.
Uamuzi wake ulifuatiwa na kujiuzulu kwa mawaziri wawili ambao waliwahi kushika Wizara ya Nishati na Madini kwa nyakati tofauti, Nazir Karamagi na Dk Ibrahim Msabaha.