Porojo: Ya Kale Hunuka

Kanungila Karim

JF-Expert Member
Apr 29, 2016
20,744
25,440
Leo nimeukumbuka tena ule uchaguzi uliofanyika zaidi ya miaka 2000 iliyopita. Mkutano wa kampeni ulifurika nyomi ya kufa mtu.

Tume ya uchaguzi (Pontius) ikawatambulisha wagombea: Mgombea wa kwanza, mtu wa hovyo kabisa, mwenye historia ya ujambazi na asiye na sera yoyote; mgombea wa pili alikuwa mtu wa maono na sera za kuwaokoa wananchi.

Kwa kutambua hatari iliyowakabili watu kama mgombea wa kwanza angeshinda, tume ya uchaguzi ikajaribu kumwengua na kumpitisha mgombea wa pili bila kupingwa.

We, wananchi wakaja juu na jina la mgombea wa kwanza likarejeshwa mara moja!

Baada ya kura kapigwa watu wakabaki hapohapo kituoni kulinda kura. Matokeo yalipotoka, mgombea wa kwanza alikuwa ameshinda ushindi wa kishindo; ushindi wa tsunami!

Mkurugenzi wa tume akawa hana ujanja, akatangaza kuwa, BARABBAS alikuwa amembwagwa YESU KRISTO kwa asilimia 100 ya kura zote! Watu wakarudi majumbani kwao roho kwatu kwa kujipatia chaguo lao!

James Gayo


119649817_3605132329517787_9052780206834920394_o.jpg
 
Back
Top Bottom