Wadau habali za majukumu nimewaletea Uzi huu ukiwa Kama ulivo ni ushuhuda WA kweli kabisa.
Nimekaa nao Kama siri lakini roho yangu imeshindwa kuamini Kama ni Mimi niliye mtendea ukatili mpenzi Wangu niliyeachana nae mnamo mwaka 2016, nilikutana nae kwa siku ya kwanza pale kituo cha daradala magomeni mapipa 2011 tukapeana Namba tukaanza mawasiliano.
Yeye alikua akiishi kinondoni mkwajuni mwisho WA siku tukawa wapenzi na kwamda mfupi tukaanza kuishi wote pale mapipa mtaa WA kionga, kiukweli nilimpenda alinipenda Sana nikamzoea kupita kiasi tulipofikisha miaka 4 hatukubahatika kupata mtoto lakini nilimpenda sikuwahi kumsumbua kwa sababu Mimi nilikua ninae mtoto huko kwetu pia hata yeye alikua na mtoto huko kwao moshi, sekeseke lilianza pale alipopata kibarua k.koo dukani kwa Mhindi hapo ndipo amani ilianza kutoweka akakutana na wachaga wenzake pale k.koo akaanza kubadilika tabia mke Wangu.
Kutokana na nilivokua nimempenda kupita kiasi nilimzoea Sana ndie mwanamke Wangu WA kwanza kuishi nae kwa miaka 4 kila siku hatujawai kutengana mambo yalizidi kuwa magumu siku moja nikiwa kazini kwang nikapigiwa cm na Mwenye nyumba akinipa taalifa kua mke Wangu anahama nyumbani,sikua na namna nilisema muache shame jioni nikaludi nikakuta kachukua nguo zake pekee vitu vyangu kaacha roho iliniuma Sana sikujari vitu niliwaza wapi nitampata mke Wang pia kujua amekwenda kupanga wapi!! Siku ya kwanza sikulala sikupitiwa usingizi sikula chakula chochote nikawa na mawazo mengi sitayasahau sijawai kuumia Kama kipindi hicho.
Nikadhoofika afya yangu maana nilikua sili chakula pia nikawa na mawazo mengi hata kazi nikafukuzwa, nikamfata ofsini kwake pale k.koo Bos akasema alishaacha kazi yapata wiki, nikachanganyikiwa Sana baada ya hapo wivu WA kikatili ulijaa kifuani nikaaza kumtafta kupitia rafiki zake ninaowajua kumbe alikwenda kupanga chumba kigogo, nikaperereza nikaijua nyumba nikaanza kumvizia Usiku, siku moja nikabahatika kumuona anaingia na Pikpik hapo kwake moyo ulipasuka nikaishiwa nguvu sikuweza hata kumuita badae nikaona inaingia Pikpik akatoka ndani ya geti mke Wangu akampokea yule jamaa mida ya saa3 usiku.
Niliishiwa nguvu wakuu nikaondoka moyo ukiwa umejaa ukatiri WA hali ya juu ulioambatana na wivu WA mapenzi mazto.