Ponyesha ndoa upate amani

timetoloveyourself

JF-Expert Member
Mar 24, 2015
206
206
ULIYE NDANI YA NDOA NA UNAYETEGEMEA KUINGIA SIKILIZA NENO HII
ROHO AWAAMBIA NINYI KUPITIA KINYWA CHANGU.......

Uchafu ni asili ya shetani, uchafu huo hautofautiani, nazungumza uchafu wa kiroho na mwili,
usidhani kwa kuwa umeshampata huyo ndiyo mwisho wako kuoga, kuswaki, kudeki, na kutandika kitanda,
napenda ujichunguze kabla ya kumpata huyo mwenza wako, ulikuwaje?
Utajikuta ulikuwa na kauli njema, ulikuwa na ahadi za kutomjeruhi moyo, ulikuwa mzabibu Mwema, leo umegeuka na kuwa mzabibu mwitu,
unavyoishi na mwenza wako sivyo ulivyokuwa mwanzo, na zaidi unajidanganya eti na wewe umeokoka!!
Ni mbingu ya nani inayowahifadhi wachafu wa roho na mwili?
Jitathimini ulivyo sasa!!
Mwanzo ulikuwa muombaji sana kabla ya kumpata Huyo mwenza wako,
leo hatakuomba huombi umekuwa mzigo wa mwenzako, inamgharimu mwenzako kuiombea family na kuiombea Ndoa,
bila aibu wewe unabomoa, tena kwa makusudi!!
Unadhani unamkomoa Huyo
mwenza wako kumbe ni unajiumiza wewe mwenyewe.na kama umeolewa na una watoto unawaumiza na kutesa hao watoto bure na hatia hiyo ipo siku utaijibu kwa Mungu kwa kuwa ni chanzo cha talaka katika ndoa yako.
kama hujui maumivu ya kuachana waulize wazazi walioachana, watakwambia na dhihaka zote walizozipata, kibaya zaidi hata Mungu umemfanya binamu yako,
mwanzo ulijinyenyekesha kwakuwa ulikuwa misri leo hii amekupandisha kutoka nchi ya utumwa unakula na kuvaa na kupendeza unajiona umaarufu umesahau kule kwenye ufukara ulikotokea,
hujasoma maandiko kile asemacho Mungu ktk torati?
Kumbu 8:11anakuonya kuwa kama ulijua umetoka misri basi jua ukikosea tena kunakupelekwa baberi,
kuliko na utumwa mbaya kuliko wa misri,!!
Kiburi cha uzima umekitoa wapi?
Kisa unaona unaweza kuolewa tena au kuoa tena unaona unacharti na watu kwenye mitandao eti wanakupenda?
Au kwasababu ukipita njiani unapewa ofa na warembo au mashugamami na mablaza man wa dunia au mashugadadi!!
unajisahau na kumsahau mwenza wako, inafika wakati hata humuagi mwezio unapoondoka kisa unapendwa na yule jamaa, au yule binti!!
Ukweli ni kwamba geuka umrudie Mungu kwa upya ufu 2:5
naye atakurejeza, naona mwisho wako ni mbaya na wakutisha, maana imenenwa kabla ya aibu , kiburi hutangulia, na kabla ya heshima, unyenyekevu huanza,
usidhani mwenza wako anapojishusha ni upumbavu, anakuonea huruma wewe na watoto mlionao na anajiheshimu ili kutunza heshima ya Ndoa yenu,

Usipende kuishi maisha kuiga ya wengine pasipo kuyaishi maisha yenu,
maana imeandikwa Mme ataacha wazazi wake naye ataambanana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja,
akiwa na maana mtayaishi maisha yenu, kwa nini upende wewe uyaishi maisha ya watu wa nje, badala ya maisha yenu,
eti wanakufundisha wengine jinsi ya kuishi ndani na maelekezo wanakupatia, nawe kwa kutokufikiri vizuri unayapokea na kuyaleta ndani bila hata kuyapima,
na mwisho yanawaharibu wewe na mwenza wako. uko ni kukosa MAARIFA maisha yenu ya ndani takeni Mungu awafundishe nanyi fundishaneni mkiwa nyumbani kwa UPENDO NA MKIONGOZWA NA ROHO MT. pale amani hutawala kwa hiyo dukuduku zote mwaga pale na mwenza wako atakuwa wazi kwako kwakuwa atakuwa yupo ktk ulimwengu WENYE UPENDO NA AMANI NA HEKIMA YA MAZUNGUMZOi,
nikiwa na maana ulimwengu huo unaamani, na palipo amani hakuna linalositilika, mpende mwenza wako mfanye awe na amani, ili kuruhusu baraka ktk family yako.
Maana uonapo adui anawashambulia nia ni kuharibu ndoto yenu,
mafanikio yenu na mipango yenu,
mjenge tabia ya kuomba pamoja,
kula pamoja
na kusindikiza kwenye sherehe au mikusanyiko mbalimbali yenye utukufu wa Mungu au kwenda pamoja nyumba za ibada
na kuongoza ktk majukumu ya kawaida isipokuwa Yale ya kimamlaka ,yaani ya kuajiliwa.
na Ndoa yenu itadumu,
pendeni kubebeana Zawadi,
zawadi hazina umri,
kila mtu anapenda kuzawadiwa na mwenza wake
jitahidini
ktk yote jifunzeni kwa Mungu aliye hai iweni wa bunifu katika Ndoa huku mkiyafanya yote ili Mungu wenu atukuzwe ktk Ndoa na wengine wakajifunza kwenu, iweni kielelezo ktk jamii na Mungu atawaheshimu, Ndoa na iheshimike na watu wote, zaidi niseme nanyi waume wapendeni wake zenu kama miili yenu, maana ampendaye mke ajipenda mwenyewe, efe 5:28
nanyi wake watiini waume zenu, kwakufanya hivyo Mungu aliye hai atawajazeni baraka ktk Ndoa yenu, Basi angalieni sana jinsi mnavyoenenda;
si kama watu wasiyo na hekima bali kama watu wenye hekima, mkiukomboa wakati,
kwa maana zama hizi ni za uovu. Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, Bali mfahamu ni nini yaliyo Mapenzi ya Bwana kuwakutanisha ninyi hata kuwafanya kuishi.

mkaimarike ktk NENO hili awaambialo roho, ili shetani akose nafasi ktk Ndoa yenu, msiache kusoma NENO na kuliishi neno, na baba wa mbinguni atawajazeni baraka na amani, hata kuwapa uzima tele.
Leo nimesimama nikiwa mama mtumishi kufundisha hili la ndoa
najua kuna ndoa nyingi zitapona......Najua nimesema na mtu hapa aokolewe.

NB. ..
MSAADA KUJIUNGA JUKWAA LA DINI.
NIMEMWANDIKIA INVISIBLE LAKINI SIJAUNGANISHWA BADO. AU KUNA NJIA NYINGINE MNISAIDIE.
 
Hakuna neno gumu kwa Mungu enyi wanandoa. Tunaamini yeye ndie alieanzisha taasisi hii tukufu ya ndoa
 
Back
Top Bottom