Pongezi Serikali ya Rais Samia kwa kutoa kiasi cha Tsh bilioni 300 kuendeleza miradi jijini Dodoma

SOPINTO

Senior Member
Oct 19, 2020
155
385
Nianze na kumpongeza mama Samia kwa uamuzi mzuri na wenye busara zenye kulenga mwendelezo wa aliyekuwa mkuu wake wa kazi , pongezi zingine ziende kwa waziri mkuu kwa tamko la utoaji wa kiasi cha bilioni 300 zitakazotumika kuendeleza miradi jijini Dodoma iliyoanza awamu ya tano na mwendazake JPM. Muendelezo wa miradi hiyo kuanzia mji wa serikali ni ishara tosha kuwa serikali bado ipo bega kwa bega na maamuzi ya kuifanya Dodoma kuwa makao makuu ya serikali.

Kwa upande mwingine tamko hili la waziri mkuu ambaye ndiye msimamizi mkuu wa issue serikali linaweza kuwa donda lisilopona kwa wale watanzania wenye akili fupi ambao mpaka sasa bado wanawaza kuwa serikali itarudi ilikotoka Dar es salaam , kutokana na miondombinu inayotengenezwa hapo Dodoma ni dhahiri kuwa kuna mikakati mikubwa itapelekwa jijini Dodoma mapema baada ya jengo la taifa (Ikulu) kukamilika.

Mpaka sasa kiasi kilitumika kuibadili Dodoma ni kikubwa sana na ili jambo ni endelevu , watanzania hasa wakazi wa Dodoma wanakila sababu ya kumshukuru JPM kwa kasi aliyotumia kubadili na kuendeleza Dodoma kiasi kwamba ni vigumu sana kuignore hatua ilipofikia.

Jambo la msingi ni matumizi sahihi ya kiasi hicho otherwise tija ya fedha hizo itakuwa nothing.
Awamu ya sita hongereni sana
 
Naskia mshaanza makato kweye Luku na Nyumba , au kwasababu mnajua kuwa hamwezi kutoka madarakani kwa box la kura ??
 
Back
Top Bottom