Pongezi sana kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Pongezi sana kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara

Deo Haule

Member
Joined
Aug 9, 2016
Posts
41
Reaction score
34
Wadau Mimi naomba nimpongeze sana tena sana,

Mkuu wa mkoa wa Manyara Makongoro Nyerere, pamoja na ile staili yake ya kama komedy hivi nimempenda sana yule baba sababu ile inamfanya azoeleke sana na wananchi pia in raisi kujua shida za wananchi wake.

Ila kuna wakuu wa mikoa wapo hata sisi wananchi hatuwajui wamejifungia tu maofisini wanasubiri ziara za viongozi wa kitaifa ndio utawaona na mfano mzuri huku mkoani kwetu hata hatumfahamu toka ateuliwe.
 
Tanzania safari ya Maendeleo bado ni ndefu Sana, ubora wa kiongozi haupimwi kwa kuchekacheka Wala kufanya sijui comedy. Kiongozi anapaswa kuhakikisha Maendeleo ya eneo husika yanapatikana.

Hao wananchi hawatakula Wala kunywa vicheko vyake. Huo mkoa una shida ya maji Sana, ahakikishe wananchi wanapata maji Safi na salama pia ahakikishe wanapata matibabu.
 
Kinachomfanya Makongoro akubalike na Watu popote pale anapokuwa ni tabia yake ya kupenda Kujichanganya na Watu, Mtani ( Chakaramu ) sana, siyo Mjivuni, Msomi, Msela, Mtoto wa Mjini vile vile halafu hapendi kusafiria Nyota ya Hayati Baba yake Kiumaarufu.
 
Pamoja na hayo yote ndugu zangu ila Mimi nasema ni bora hata huyo wananchi wake wanamuona kuna wakuu wa mikoa jamani hawaonekani kwa wananchi wala japo kusikiliza hata kero za wananchi huwaoni mfano Mimi nipo mkoa mmoja hivi huku kusini magharibi kama unaelekea Kigoma yani huyu mheshimiwa tunamsikiaga tu kwenye Tv au kama kuna ugeni wakitaifa kweli jamani hata kama sababu ni uvico lakini mbona baadhi yao tunawaona mikoani kwao
 
Back
Top Bottom