Pongezi kwa kamanda Siro

kijana wa leo

JF-Expert Member
Nov 28, 2011
2,916
7,164
Naomba kwa moyo wa dhati kabisa nitoe pongezi zangu kwa huyu kamanda wa kanda maalumu ya Dar na nazidi kumuombea afya njema na uhai mrefu. Haya ni baadhi ya yaliyonifanya nitoe pongezi kwake,
  1. Ameweza kudhibiti ujambazi kwa kiasi kikubwa sana, ambapo leo nimesikia ndani ya week 1 amekamata majambazi 63 na silaha za moto.
  2. Ndani ya uongozi wake jeshi la police limekua likitoa ushirikiano wa haraka sana wanapopewa taarifa juu ya matukio ya uhalifu, na wamekua wakifika maeneo ya tukio kwa wakati tofauti na ilivokua mwanzo.
  3. Ameweza kukamata watu wanaojihusisha na madawa ya kulevya, wengi tumeshuhudia hadi wale untouchable wamekamatwa na wako under arrest.
  4. Anapotoa taarifa kwa vyombo vya habari anakua na umakini na anaongea kwa fact na hisia kiasi kwamba hata mtu ukiwa chizi kiasi gani utaelewa huyu mtu ana nia ya dhati na amani ya jiji la dar.
  5. Utendaji wake umeibua waalifu wengi na mitandao yao na amejitahidi kuwadhibiti.
Kwa hayo anahitaji pongezi, sasa jiji la Dar linaweza kuwa sehemu salama zaidi na hata matukio ya kuporwa pesa ukiwa unatoka/unaenda bank yataisha kabisa.
 
Kova alikuwa mtu wa TV zaidi lakini on the ground jamaa walikuwa wanafanya vitu vyao!!
 
Back
Top Bottom