Pongezi kwa jeshi la polisi na Kamanda Kova | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pongezi kwa jeshi la polisi na Kamanda Kova

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Magezi, Aug 25, 2009.

 1. M

  Magezi JF-Expert Member

  #1
  Aug 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Majambazi NMB Temeke yanaswa

  • Yumo askari wa JWTZ kikosi cha Mgulani

  na Sophia Maghembe  SIKU chache baada ya Jeshi la Polisi nchini kutangaza donge la sh milioni 5 kwa watakaofanikisha kutiwa mbaroni kwa majambazi waliovamia Benki ya Taifa ya Microfinace (NMB), tawi la Temeke, jijini Dar es Salaam, tayari watuhumiwa 13 wamekamatwa kwa nyakati tofauti.

  Akizungumza jana na waandishi wa habari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Msaidizi, Suleiman Kova alisema, wamefanikiwa kuwakamata watuhumiwa hao, akiwemo askari wa Jeshi la Wananchi (JWTZ). Watuhumiwa hao wamekamatwa wakiwa na magari manane pamoja na bunduki mbili.

  Aliongeza kuwa, walikuwa na bastola moja na SMG iliyoporwa kwa polisi mmoja siku ya tukio.

  Kova aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni askari wa JWTZ SGT Mathew (42), mwenye namba MT 55935, mkazi wa Kibaha, Musa Abdallah (30), mkazi wa Yombo Buza jijini Dar es Salaam na Obadia Gabriel (23) waliokufa katika mapambano na polisi wakati wakijihami.

  Wengine waliokamatwa ni Antony Jeremia (30), mkazi wa Dodoma, Issack Swai, maarufu kama Fataki (23), Deogratus Masawe (30) ambao ni wakazi wa Moshi, Salum Yasin maarufu kama Jibaba (28), Yusuf Rajabu (44), Boniface Joseph (34), Japo Salimu (27) na Saidi Hamisi (30), wote wakazi wa jijini Dar es Salaam.

  Aliongeza kuwa, watuhumiwa wawili ambao hakuwataja kwa majina kwa sababu za kiupelelezi, mmoja yupo Arusha na mwingine Kigoma.
  Wengine wawili wapo Kituo cha Polisi Kati jijini Dar es Salaam ambapo magari yote yatafikishwa jijini Dar es Salaam kwa utambuzi kujua wamiliki wake halali.

  Alisema watuhumiwa wote watafikishwa mahakamani kujibu mashitaka yanayowakabili, na wengine wawili ambao hawajatambulika, watatambuliwa hivi karibuni katika gwaride la utambulisho baada ya upelelezi kukamilika.
  Katika tukio hilo, majambazi saba walivamia benki hiyo na kurusha mabomu matatu ya kutupwa kwa mkono na kuua mlinzi wa kampuni binafsi ya ulinzi, Seif Mwikwike, kujeruhi wengine wanne na kupora sh milioni 60.

  Source: Tanzania Daima
   
 2. Zogwale

  Zogwale JF-Expert Member

  #2
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 10, 2008
  Messages: 11,613
  Likes Received: 825
  Trophy Points: 280
  Hivi watafanikiwa kuwafunga??!! Au ni kutuzuga tu!! Naomba mwenye taarifa ya maendelea ya ile kesi ya uporaji NMB pale mataa ya ubungo atudondoshee hapa. Kulikuwa na kesi ya wizi pale kisutu na ile ya mauaji mahakama kuu. Ile ya wizi kisutu nasikia walipatikana na makosa ya kujibu. Je hukumu je?? Na ile ya Mahakama kuu April 2009 kulikuwa na hearing, je imekomea wapi hatujui. Hivi ni kweli kuwa wenye feza hawafungwi!!! Labda kweli!!! I am kiding!!!!!
   
 3. M

  Malyamungu JF-Expert Member

  #3
  Aug 25, 2009
  Joined: Jul 5, 2009
  Messages: 363
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Watafungwa vp wakati wabunge wakienda bungeni wao ni kuongea ufisadi mpaka wanasahau kutunga sheria za ufisadi na ujambazi huku polisi wetu wakiuawa bila makosa. Hapa ni jambo la kisiasa lahitajika to put policies in force, kutunga sheria au kuweka vizingiti vya sheria hizo na siyo kuwanyima au kuweka dhamana ngumu kwani linajitokeza sana kwenye kesi nyingi kwa muda wa miaka ya hivi karibuni.

  Yatakiwa itungwe sheria inayokndamiza haswa na ndiyo maana wezi watoka kenya na kwingineko kwani bongo shamba shakua la bibi.
   
 4. M

  Magezi JF-Expert Member

  #4
  Aug 25, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli hata mimi nacho kiona ni bunge kuwa busy na mambo mengine na kusahau kutunga sheria kali dhidi ya majambazi na wezi wengine, wauaji albino n.k.
   
Loading...