Pongezi kwa halmashauri ya mji wa Babati

Pongezi kwa halmashauri ya mji wa Babati

christeve88

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2018
Posts
3,338
Reaction score
5,492
Kwanza nianze kuwapongeza kwa wazo lenu nzuri la kujenga stendi mpya eneo la Makatanini nje kidogo ya mji wa Babati.

Wasiwasi wangu na wananchi walio wengi hususani wa mji wa Babati ni udogo wa hiyo stendi, hapa mtanisamehe wadau kwa kushindwa kuchukua picha maana sikuwa na simu janja wakati napita eneo hilo. Kwakweli stendi ni ndogo sana yaani ni kama ya mji mdogo wa magugu japo nayo maduka yaliyozunguka hiyo stendi yamepauliwa hovyohoyo tu mara mengine paa refu mengine fupi ilimradi liende.

Nikiwa kama mdau wa maendeleo nilijaribu kuuliza baadhi ya wadau kwa nini halmashauri imeamua kujenga stendi ndogo hivyo wakati wanajua fika kuwa Licha ya Babati kuwa makao makuu ya mkoa wa Manyara, Babati ni njia panda ya kwenda Dodoma na Singida, pia Babati imepitiwa na barabara ya C to C yaani Cairo to Capetown kwa hiyo muda sio mrefu Babati itaanza kupitisha magari mengi sana hasa Baada ya Serikali kuhamia Dodoma na kukamilika kwa barabara ya babati Kondoa Dodoma, wadau wengi wanasema hawajui sababu na wengine wanadai kuwa eneo la kujenga stendi ni kubwa sana ila wanashangaa kuona inajengwa ndogo.

Sasa kwa hali ilivyo, na kwa umuhimu wa hiyo barabara mtalazimika kupanua hiyo stend ndani ya miaka miwili gharama ambazo mngeweza kuziepuka sasa. Ni vyema tukaiga mfano wa stendi bora kama ya Morogoro, Singida, Korogwe na Mpanda.
 
Nimepita Iringa,Kibaha na Babati stendi zao zipo kwenye muundo huo. Sijui ni kwa nini serikali inapoteza hela kwenye vitu ambavyo kwa hali ya kawaida haikizi vigezo.. Wanatakiwa waende kujifunza kwa stendi za Korogwe na Singida.
 
Dah! Pale Baba T patamu pale... Nikipata nafasi nitarudi tena. Probably this Dec... I have unfinished business there...
 
Morogoro,Korogwe,Singida,Kange Tanga(angalau) na Mpanda..ndio stendi bora Kwa sasa.
Kuna vitu hata hutumii utaalamu unagundua tu. Hawa Tamisemi na miradi yao ya ULGSP wanatakiwa kujitafakari upya.. Hizo hela ni za mkopo na tutakaolipa ni sisi wananchi.
 
Back
Top Bottom