Pongezi Kwa Dada Rose wa Kitengo cha Huduma za Dharura TANESCO

Amavubi

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
30,156
13,249
Moja ya Kazi za lawama sana ni eneo la kushughulika na watekja na ni eneo ambalo Tanzania imelaumiwa sana na kiukweli eneo lenye lawama lukuki kwa Taasisi, Makampuni na Mashirika ya umma na Binafsi hata wengine wamelazimika kufunga ving'amuzi kubaini wateja wanaohudumiwa istahilivyo

Nimekuwa nikipiga simu mara kwa mara kitengo cha dharura TANESO na hata hapa niliwahi kuleta mada ya LUKU na nimekua nabahatika kukutana na dada Rose na mara nyingi hujitambulisha kwa jina moja la Rose kwa kweli nitakua mnyimi wa fadhila bila kumrushia pongezi dada huyu kwa jinsi anavyomudu kazi yake kwa majibu ya upole na uhakika na jinsi anavyofuatilia tatizo lako kuhakikishia umepata huduma stahiki

hongera sana dada Rose mpo wachache sana nchi hii

aidha niwatime shime wahudumu wengine wa vitengo kama hivyo jinsi wateja wanavyoumia pale wanapokosa kile wanachostahili, nadhani imefika wakati hata wateja hawaoni umuhimu wa kupiga simu sababu wanajua tu kwamba ni kupoteza muda wao

my best wishes goes with her
 
Vipi kuhusu customer care ya mtandao wa tigo?.
mhhhhh I reserve my comments..................ingawa wapo ambao sometime yes ingawa yamkini wanajitahidi kuboresha ila ninachogundua kwa hizi cellular company wana masilahi duni sana kutokana na mikondo mingi ya walaji na hii huathrii watendaji kisaikolojia hata kushindwa kutoa huduma kwa ufanisi chengine ni nepotism yaani undugunaizesheni kwenye hizo ajira watu wanaajiriwa si kwa ujuzi ama uzoefu bali kwa kujuana ....nawasihi wajitahidi kuboresha pia
 
Last edited:
Hongera dada rose ingawaje hajasema ni tanesco ipi endelea na kazi nzuri
nadhani itakua ya mikocheni maana ndio nipo jirani ila hiyo ni namba ya huduma kwa wateja wa dharura
 
Back
Top Bottom