Pongezi David Nzela

Idd Ninga

JF-Expert Member
Nov 18, 2012
5,208
4,406
1>mungu akupe maisha,marefu yenye
baraka.
Lugha vyema wafundisha,twaelewa
kwa haraka.
Njia umetuonyesha,nasi twapenya
kichaka.
Pongezi davidi nzela,mema
ninakuombea.
2>ushauri na nasaha,zako
tunazingatia.
Tunajawa na furaha,moyo unapotutia.
Kwako jawa na furaha,huzuni
hutofikia.
Pongezi davidi nzela,mema
ninakuombea.
3>mungu akupe marifa,akujaze na
busara.
Ajalie nyingi sifa,iwe ndie yako sira.
Wanafunzi wawe zafa,wawe wema
kwa hadhira.
Pongezi davidi nzela,mema
ninakuombea.
4>fundisha kwa moyo wote,na
fundisha watu wote.
Na tumia muda wote,kufundisha yale
yote.
Unachojua chochote,kitumie kwa
lolote.
Pongezi davidi nzela,mema
ninakuombe.
5>mungu ajaze imani,aisambaze
moyoni.
Uamini kwa yakini,sali humu duniani.
Zaidi kuwa makini,asikupate shetani.
Pongezi davidi nzela
,mema
ninakuombea.
SHAIRI=pongezi davidi nzela.
MTUNZI=Iddy Ninga wa Tengeru
Arusha.
0765382376.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom