Pombe inawaangamiza vijana

Pombe inawaangamiza vijana

Mwanapropaganda

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2014
Posts
4,235
Reaction score
2,512
Licha ya kuwa maisha ni magumu, vijana wengi wa sasa nchini Tanzania ni watumiaji wakubwa wa pombe tena zile zilizo kali.
Nakutana na vijana wanadai kuwa pesa ni ngumu na wakati mwingine wanadiriki kukuomba ukidhani kuna cha maana wanafanya kumbe ni kwenda kununulia pombe.

Hali hii ilizoeleka kuwa ni vijana wa mitaani walioshindwa kwenda shule ndio wanajihusisha na matumizi ya pombe kumbe upepo umebadilika na sasa hata wasomi wa vyuo vikuu wamekuwa ni watumiaji wa vileo.

Nimefanya uchunguzi usio na shaka na kubaini kuwa vijana wengi wa sasa wanaotumia vileo ni wale wenye umri wa kuanzia miaka 17 kwenda juu na wengi wao wakiwa ni wanafunzi wa taasisi za elimu ya juu.

Kwa vyovyote iwavyo hili ni tatizo ambalo linachangia kurudisha nyuma maendeleo ya vijana na taifa la kesho.
Nadhani kuna watu wameliona na wanaliona hili, wewe kama mzazi/mlezi una mpango wa namna gani wa kumuepusha kijana wako asijiingize kwenye tabia mbovu ya unywaji wa pombe?

Tusemezane
 
Umeongea pointi mkuu, Serikali ingefumbua macho na kupiga marufuku pombe kali kupakiwa kwenye mifuko ya plastic kama walivyopiga maji ya kandoro.

Vv
 
kunywa pombe kunarudisha maendeleo ya taifa nyuma??
 
Kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako
 
sidhani kama kuna namna yoyote ya kumfanya kijana asinywe, ni decision yake mwenyewe, omba tu awe na hekima..mi wazazi wangu hata hawakuniambia kuhusu kunywa pombe, its a lesson nilijifunza mwenyewe, nilikunywa, nikapunguza hadi sasa sinywi pombe ya aina yoyote na ninamshukuru Mungu, somethings ni mtu kujifunza mwnywe,wangapi mliambiwa msinywe na bado mnakunywa hadi kulala?! unaweza ongea hadi kulia lkn mwishowe decision ni ya kijana mwenyewe
 
Dah! Umeongea tupu mkuu. Suala la kuacha pombe ni la mtu binafsi, kuna watu wanajifanya eti wana dawa ya mtu kuacha pombe! Wizi mtupu
 
Mkuu nawe unaonekana tatizo hili limekuadhiri kwa kuwa ili utafiti usiwe na shaka ni lazima uishi mazingira halisi ya unaowatafiti,upige vyombo kama wao!
 
Kunywa pombe kupita kiasi ni hatari kwa afya yako

Kwa umasikini uliokithiri kwa watanzania walio wengi kuna ulazima wa kunywa pombe kweli? watu hata milo mitatu hawaipati lakini pombe wanakunywa, kwanini hiyo gharama wasiitumie kugharamia chakula kizuri hata kwa mlo wa usiku tu?
 
pombe inarudisha nyuma maendeleo? wabunge walilia sana kodi iongezwe kwenye pombe na sigara na si mafuta,wakitambua kwamba ndo kimbilio siku zote la bajeti ya Tanzania wee
 
Mkuu nawe unaonekana tatizo hili limekuadhiri kwa kuwa ili utafiti usiwe na shaka ni lazima uishi mazingira halisi ya unaowatafiti,upige vyombo kama wao!

Hapana ila ninakerwa na vijana wanakunywa pombe huku hali zao za kimaisha zikiwa duni sana na wengi wakiwa bado ni tegemezi.
 
Wanasiasa na siasa ndio hurudisha maendeleo ya taifa nyuma...Pombe hizi hizi ndo zinasababisha watoto wa wenye mamlaka za kisiasa kufanya kufuru!

Pombe inasababisha watt wa vigogo kufanya kufuru kivipi mkuu..??
 
Hapana ila ninakerwa na vijana wanakunywa pombe huku hali zao za kimaisha zikiwa duni sana na wengi wakiwa bado ni tegemezi.

Ukiona hivi ujue kuna mahali mfumo tawala umekosea! Suala la elimu lisingekuwa huria na serikali ikaweka sheria kali kwamba vijana wote wenye uri wa kuanza shule ni lazima kupata elimu hiyo kwa uwezeshwaji wa serikali hadi kufika walao shahada ya kwanza halafu mifumo ya ajira rasmi na zisizo rasmi ukawa imara hawa vijana ungewaona wapi kwenye ungwaji usiofaa?
 
Back
Top Bottom