Mkuu nadhani wazungumzia ulevi haswa haswa.., maana huwa kuna wanywaji wa pombe na walevi wa pombe!
Swala la ulevi linaelekea kuwa janga la taifa na pengine niseme hauhitajiki utafiti wa kisanyansi kuhakiki hili.
Mitaani mwetu kumejaa vijana walevi wa kupindukia. Mfano mzuri ni asubuhi ukitupia macho kwenye vibaraza vya maduka tayari vijana wana viroba/banana.., wengine wameshalewa tayari!
Pita jioni, mara nyingi utawakuta wengi wao wako pale pale!
Jiulize swali, nguvu kazi ya taifa wanawajibika saa ngapi kujiingizia kipato cha kujikimu na kulewea!?
Je kwa style hii tutakuwa na taifa la aina gani huko mbeleni?
Wenzetu Kenya wako kwenye kampeni ya kupiga vita ulevi kwa maana wameshatambua kuwa ni janga.., kazi kwetu kusemezana na vijana wetu wapunguze ama kuacha ulevi kabisa!!