Yyyyesss!
Sisi tuliochelewa kimaendeleo, tunahitaji kuwaiga wachina na labda zaidi ya wachina ktk kutekeleza mambo muhimu kwa ajili ya maendeleo ya taifa hili, uzuri Magu anatekeleza majukumu yake kwa kufuata sheria, wahanga wengi wa hatua zinazochukuliwa sasa na serikali ya Magu ni wale walifanya mambo yao kiholela tofauti na maadili ya taaluma zao, ama kwa raia wa kawaida ni wale waliofanya mambo kinyemela huku wakijua bila kufuata utaratibu, na wengine kwa ujinga wao tu.
Rais anaweza kuonekana anakiuka haki za binadamu lakini kimsingi makosa hayo yalifanywa na watangulizi wake kwa kuacha mambo kiholela, lazima turudi ktk misingi, kwa bahati mbaya maendeleo ktk sehemu nyingi ulimwenguni ktk nchi zilizochelewa yaligharimu raia wake hasa wa aina nilizozitaja hapo juu.
Kwa swala la bomoabomoa watanzania waishio mabondeni walishapewa taarifa miaka nenda rudi, lakini ndo kwanza waliendelea kujenga kwa mazoea yaleyale!
Hivi kipi bora, kuweka utaratibu wa kuwa na helkopta za kuokolea wakati wa mafiriko na kupoteza maisha ya watu
AU
kuwahamisha wakaishi salama maeneo salama? Nijuavyo hadi ss zoezi la bomoabomoa halijasababisha kifo kwa mtu yyte, lkn mafuriko yaliyotangulia yamegharimu maisha ya watanzania wengi.
Ila kwa kuwa wengine sie ni wapingaji wa kila kitu tupingeni tu, siasa uchwara zimechelewesha sana maendeleo ya nchi hii.