Polisi yavuna mil. 316 faini magari

Polisi yavuna mil. 316 faini magari

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
28,197
Reaction score
64,639
558edaf60a3a5768a43a7e1a271a0212.jpg

JESHI la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, kupitia Kikosi cha Usalama Barabarani, limekusanya zaidi ya Sh. milioni 316.6 ndani ya siku mbili kutokana na oparesheni ya ukamataji wa magari yanayokiuka sheria.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa, alisema mbele ya waandishi wa habari jana kuwa operesheni hiyo iliyofanyika kwa siku mbili hadi juzi, imewezesha kukasanya kiasi hiko cha fedha.

Alisema katika operesheni hiyo magari yaliyokamatwa kuwa ni 10,253 na pikipiki zilikuwa 404.

Alisema katika operesheni hiyo inayoendelea pia walikamata daladala 3,990 na magari binafsi na malori 6,263.

Aidha, Mambosasa pia alisema kutokana na operesheni hiyo, madereva wa bodaboda 44, walifikishwa mahakamani kwa makosa ya kutovaa kofia ngumu (helmet) na kupakia zaidi ya mtu mmoja, maarufu kama mishikaki.

Sambamba na hilo, alisema jeshi hilo liliwaua watu watatu wanaosadikiwa kuwa majambazi kati ya watano ambao walipanga
kuvamia na kupora katika maduka ya M-Pesa na Tigopesa, maeneo ya Mbiku Chamazi.

“Tulipata taarifa za mipango hiyo ya majambazi na askari wetu hatimaye waliweka mtego na walifanikiwa kuwaona majambazi hao wakishuka kwenye gari lao kwa ajili ya kufanya tukio hilo,” alisema.

Alisema majambazi hao walianza kufyatua risasi kuwashambulia askari baada ya kugundua wanafuatiliwa na askari walijibu mashambulizi na kufanikiwa kuwajeruhi watatu kati ya watano huku wengine wawili wakikimbia.

“Majambazi waliojeruhiwa walifariki dunia baada ya kufikishwa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa ajili ya matibabu na msako mkali unaendelea kuwatafuta majambazi wawili waliokimbia,” alisema Mambosasa

Chanzo: Nipashe
 
Chanzo kizuri cha mapato,kama siku mbili ni 0.3b maana yake kwa mwezi wanakunja 4.5B
 
Ningeomba jeshi la polisi litoe semina Kwa Raia wala wasichoke kwa Hilo mfano speed uko 42 na unafaa uwe speed 40 jamani kweli hapo unakula fain unalipa huku ukinung'unika ambayo kwakweli jeshi la polisi mko vizuri sana na ukweli ajali imepungua sana mungu ibariki Tanzania na watu wake ameen
 
Hapo na rushwa wamechukua kunguru hao. kuna sehem walitaka buku tano nkawabambikia elf2 mpya kisa wiper
 
Back
Top Bottom