Polisi yavamia harusi, wakamata bwana harusi na watu wake na kupewa kesi ya ujambazi Access Bank

Jindal Singh

JF-Expert Member
Sep 9, 2015
1,857
1,538
Baada ya kupitapita huku na kule katika maeneo yaliyotokea kadhia ya ujambazi jana nilifanikisha kunasa tukio Moja maeneo ya Chulwi Kongowe Mbagala kama sijakosea.

Mnamo 27.2.2016 majira ya SAA 12 jioni polisi walivamia harusi iliyokuwa ikifungwa msikitini na kuwakamata watu waliokuwemo ndani wakiwatuhumu kuhusika na Ujambazi uliofanywa siku ya tarehe 26.2.2016 katika tawi moja la Bank ya Access lililoko Mbagala.

Raia walisema polisi ilivamia msikiti na kuwakamata walimu wa dini waliokuwa wakifungisha ndoa hiyo na kuwachukua na kwenda nao hadi ilipo harusi na kuwakamata wengine huku wakiwapiga na kuwatuhumu kuwa wamehusika na ujambazi.

Hata hivyo polisi ilimwachia huru bibi harusi na kuondoka na babu harusi na wapambe wake sehemu kusiko julikana.

Miongoni mwa watu waliokamatwa ni Abdullah Saudi, Juma selemani, Saidi Ally na kassimu Othuman wote wakiwa wakazi wa Mbagala waliokuja kusheherekea harusi ya rafiki yao.
 
Sasa Mbona Hizo Tarehe Za Matukio Zinaleta Ukakasi!!? Jana Yake Tu Wanauwa Na Kupora Mapesa, Kesho Yake Anaoa Mke!! Ina Maana Hizo Walikuwa Wakiziratibu Vp Kwa Wkt Mmoja!!? Na Wakafanikiwa Zoote!!!!!!!??? Kuvamia Bank Ni Mchakato Wenye Kuhitaji Muda, Kupanga Huo Mkakati Na Kuutekeleza, Na Harusi Ni Mchakato Pia Unahitaji Muda Kupanga Mambo, Na Kutekeleza!! Sasa Huyo Mtu Alikuwa Akitekeleza Vp!!!!?? Kama Ni Huko Watuhumiwa Kukimbia Kuelekea Eneo Lao Tu, Ndio Kimetokea Hicho, Itakuwa Sio Sawa!!
 
INTERMISSION ...... S. SIRO anaweza kuwa hata zaidi ya TIBAIGANA Na KOVA ....
 
Back
Top Bottom