Polisi yasitisha kuwabebesha madereva mabango ya makosa yao

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,411
Kamanda wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga amesema wamesitisha kuwatangaza watuhumiwa katika mitandao ya kijamii baada ya kupata malalamiko ya Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Hata hivyo, amesema hadi wanasitisha walikuwa wamewakamata madereva 20 wa Dar es Salaam, lengo likiwa ni kuonyesha jamii ili wengine wenye tabia hiyo wajifunze kupitia kwa wenzao na kuacha kuendesha wakiwa wamelewa.

“Kwa sababu watu wengi wapo mtandaoni ilikuwa rahisi ujumbe kuwafikia kwa wakati mmoja. Tulipata malalamiko ya haki za binadamu kuwa kufanya hivyo kunawasababishia kudhalilika katika familia zao, tukaona tusitishe,” amesema Mpinga.

Amesema pamoja na kusitisha utaratibu huo, madereva wasijisahau kwa sababu vijana wapo kazini na wanaendelea kuwakamata wale wote watakaokiuka sheria za barabarani, ikiwamo hiyo ya kuendesha wakiwa wamelewa.

Awali, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora imelitaka Jeshi la Polisi, Kikosi cha Usalama Barabarani, kuacha kuziweka hadharani picha za madereva wanaotuhumiwa kukiuka sheria, badala yake liwafikishe mahakamani kwanza.

Kauli ya Tume hiyo imetokana na utaratibu ulioanzishwa na trafiki wa kuwavisha mabango madereva wanaotuhumiwa kukiuka sheria ambayo yameandikwa makosa yao na kurushwa kwenye mitandao ya kijamii kabla hawajafikishwa mahakamani.

Mwenyekiti wa Tume hiyo, Bahame Nyanduga amesema hayo wakati akifafanua kuhusu kusitisha kuwaanika katika mitandao ya kijamii madereva wanaokamatwa na trafiki kwa makosa ya usalama barabarani ikiwamo ulevi.

Chanzo: Hivi Sasa
 
Kwahyo kuwabebesha mabango waliamini ni njia sahihi ya kupambana na matatizo ya madereva wawapo barabarani?
 
Nampongeza kwa dhati kabisa kamanda Mpinga kwa kuwa hajayabeba madaraka yake kichwani, wala hadhani kuwa ukiwa kiongozi mara zote utakuwa sahihi.

Ameshauriwa na tume ya haki za binadam, ameona utekelezaji wa ushauri huo haileti madhara kwa jamii bali inasaidia kukuza na kuboresha heshima ya mtuhumiwa.

HONGERA KAMANDA MPINGA.

Pendekezo:-
Kama watanzania wengi hawapendi kutozwa faini kwa makosa ya barabarani basi wafungwe jela miezi mitatu (taratibu za kuwafunga ziwe za kisheria)
 
Kama ilisaidia kupunguza makosa ya barabarani bàsi waendelee kuwavisha mabango baada ya kuhukumiwa mahakamani
 
Back
Top Bottom