Polisi yaruhusu maandamano ya Dr Slaa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Polisi yaruhusu maandamano ya Dr Slaa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Serayamajimbo, May 1, 2009.

 1. S

  Serayamajimbo Senior Member

  #1
  May 1, 2009
  Joined: Apr 15, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatimaye baada ya Polisi Mkoa wa Iringa kukataa kuruhusu maandamano ya Dr Slaa toka jana. Muda mfupi uliopita wameruhusu maandamano hayo yafanyike kesho jumamosi Mei 2, 2009 kuanzia saa 3 asubuhi. Maandamano hayo yataanzia uwanja wa Mwembetogwa.

  Kwa mujibu wa barua ambayo waombaji wameiwasilisha kwa kamanda wa polisi maandamano hayo yanataka mishahara na maslahi ya viongozi wote wa umma wenye nyadhifa za kisiasa yajulikane kwa wananchi kama alivyosema Dr Slaa. Pia waandamanaji hao wanapinga nyaraka za wizi na ufisadi kuitwa za siri halali za serikali. Pamoja na mambo mengine wanalaani ufisadi na usimamizi mbovu katika mgawanyo wa mbolea ya ruzuku na kupanda kwa gharama ya pembejeo katika taifa hali inayoathiri kwa kiasi kikubwa maisha ya wakulima. Mkoa wa Iringa ndipo ambapo kulitangazwa azimio la "Siasa ni kilimo" lenye lililolenga kuwakomboa watanzania ambalo watawala wa sasa wamelipuuza.

  Katika tangazo lao, viongozi hao wameeleza pia kuwa mwisho wa maandamano hayo watanzania watakaoshiriki watasimama kwa ukimya kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu waliofariki katika milipuko ya mabovu katika mkoa wa Dar es salaam.

  Mwenyekiti wa CHADEMA, Manispaa ya Iringa mjini Mchungaji Msigwa ambaue ni mmoja wa wajumbe katika kamati ya wananchi ya maandalizi ya maandamano hayo, ametoa mwito kwa wanachi wa Iringa kuhudhuria kwa wingi na kwa wale wenye kuhitaji maelezo zaidi wawasiliane nae kupitia namba yake ya mkononi 0754360996. Shime mtanzania, huu ni wakati wetu wa kuleta mabadiliko

  Serayamajimbo
   
 2. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #2
  May 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Mualikeni Seif Sharif ili awasaidie kurapu ,mpeni kama nusu saa tu ,muone atakavyowasha moto huko ,ila Sultani CCM akijua kama mtampa ukumbi basi wanaweza kuondoa kibali cha maandamano hayo ,kwani wanamuelewa vyema huwa hana sumile kwa walioko madarakani.
   
 3. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #3
  May 1, 2009
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  naona wanamtega slaa ili wamuharibie katikati ya maandamano.
  kila la heri slaa na wazalendo wote
   
 4. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #4
  May 1, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,086
  Likes Received: 1,733
  Trophy Points: 280
  Hamad, Seif Sharif is hypocrite.
   
 5. Chapakazi

  Chapakazi JF-Expert Member

  #5
  May 1, 2009
  Joined: Apr 19, 2009
  Messages: 2,881
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ki-vipi?
   
 6. AnnaPeter

  AnnaPeter New Member

  #6
  May 1, 2009
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 1
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumuunge mkono Mesimiwa Dr. Slaa, maana anachokifanya ni kwa ajili ya watanzania wote kama sio wengi, tusikamane sote kwa pamoja.
   
 7. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #7
  May 1, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Dr Slaa for the Presidency!!
   
 8. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #8
  May 1, 2009
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,691
  Likes Received: 82,610
  Trophy Points: 280
  Hongera sana Dr Slaa Watanzania wengi tuko bega kwa bega katika mapambano haya magumu dhidi ya mafisadi. Pia tusisahau kumuunga mkono shujaa wetu mwingine Mengi ambaye sasa hivi Watetezi wa mafisadi ndani ya serikla na CCM na mafisadi wenyewe wanamshambulia kwa speed ambayo si ya kawaida.

  Alutta Continua
   
 9. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #9
  May 1, 2009
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Ingewezekana kama kuna njia yeyote wanajf tungejitahidi kuwahamasisha wenzetu wa Iringa[ kutoka wilAya zote] wajumuike kwenye maandamano hayo kwa niaba ya walalahoi wadanganyika wote!!Kwako INVISIBLE na MWANAKIJIJI kama kuna namna yeyote ile ya kuhamasisha haya maandamano.
   
 10. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #10
  May 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Slaa bado kuweza kuhimili vishindo vya Uraisi hata mwenyewe alisikika akidai kuwa hajawa tayari ,kwa maana kwenye Urasi kunahitajika mtu safi ,nina wasiwasi Slaa ana matatizo ambayo anayahisi yamempa sababu za kutokuwepo mstari wa mbele kuhusiana na nafasi hiyo ndio ameamua kurudi katika ubunge ,ila kama Chadema for that nafasi sio mbaya alimuradi Sultani CCM awekwe benchi na kuangali namna gani Nchi inatakiwa kuendeshwa na kushugulikiwa sio kama wanavyoishugulikia wao kimchwa :D
   
 11. B

  Bobby JF-Expert Member

  #11
  May 1, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mwiba sorry huenda sijakusoma vizuri hivi kwani JK ana nini cha kumzidi Dr. Slaa? Mbona mimi sikioni na the way nchi inavyoendeshwa kienyeji I even have a feeling kwamba mtu yeyote anaweza kuwa rahisi (rais) wa nchi hii though sikuwahi kufikiri hivyo kabla ya hii awamu ya kisanii.
   
 12. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #12
  May 1, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Wewe unataka afanye lipi ili ujue kama ana uwezo wa kuhumili vishindo? Sijawahi kuona mwanamume ambaye amewahi kuhimili vishindo kama Slaa. Kawataja mafisadi pale mwembe yanga, akalia na Richmond, akafichua Kiwira na Mkapa (Mkapa kufanya biashara Ikulu) etc etc. Sura ya nchi kupigana na ufisadi, hii leo bila ya Slaa ingekuwa ndoto, hata neno ufisadi limetumika kiu-fasaha zaidi baada ya Slaa kuanza kulitumia. Huyu ndiyo can really bring change for our country!

  Slaa for the Presidency!!
   
 13. B

  Bobby JF-Expert Member

  #13
  May 1, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Mwiba sorry huenda sijakusoma vizuri, hivi kwani Jk ana nini cha kumzidi Dr. Slaa mbona mimi sikioni? Infact the way nchi inaendeshwa kienyeji I even have a feeling kwamba mtu yeyote anaweza kuwa rahisi (rais). Sikuwahi kufikiri hivyo b4 except katika awamu hii ya kisanii kwa kwenda mbele.
   
 14. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #14
  May 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Anhaa ,inaonyesha mna jazba.Na hamjazisoma siasa na kuwasoma wahusika vilivyo,hilo sio langu bali yeye mwenyewe alisikika akisema hayupo tayari kugombea,sina kumbukumbu ya wapi na lini lakini JF wapo watu vichwa ambao wanaweza kukuonyesheni hilo.
   
 15. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #15
  May 1, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  Yahe umechemsha hapo!
   
 16. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #16
  May 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Huenda ikawa kundi kati ya makundi ya Sultani CCM yanamtumia katika kuzamishana,ndio maana yake ,kesi ya kuwekewa vitega sauti imefikia wapi ,fungueni macho na muone ,eti kawataja ,nakubaliana kuwa kawataja ,na hata Mengi nae amewataja na wengine wanawataja.
   
 17. I

  Interested Observer JF-Expert Member

  #17
  May 1, 2009
  Joined: Mar 27, 2006
  Messages: 1,401
  Likes Received: 434
  Trophy Points: 180
  yaheee, tumemwachia Seif tangu mwaka 1995 hajafanya lolote, sasa waachie na wengine wajaribu ati!

  SLaa the Presidency!!
   
 18. B

  Bobby JF-Expert Member

  #18
  May 1, 2009
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,682
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 160
  Wala si jazba Mwiba kwani wewe hupo Bongo? Sorry, but this is very true, miaka ya nyuma nilikuwa niko very proud kutangaza utaifa wangu nikisafiri nje ya nchi lakini sasa nisipoulizwa hata sitaji utaifa wangu naona aibu sana. Nchi inaendeshwa kama nini sijuwi nakosa hata mfano. Can you imagine tuko na sheria za aina 2 sasa, za walalahoi na wenye nacho. Mwenye nacho anaweza kufanya lolote na chochote kisifanyike kwake. Waziri anaweza kufanya lolote hata rushwa iliyothibitishwa na still akaendelea kuwa waziri.Bunge linatoa azimio kwa serikali (Hosea na Mwanyika) hakuna chochote kinafanyika. Do we really have a government au usanii tu? Binafsi ninaona aibu kwelikweli kuwa mtz kwa sasa.

  Hayo ni machache tu Mwiba the list goes on and on. So kipi kitamshinda Slaa hapo?
   
 19. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #19
  May 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Ukisema hajafanya lolote utakuwa unajenga dharau ,hao unaowasifia wamefika hapo kwa namna Seif anavyoinyanyasa na kuikaba serikali iliyopo madarakani ,Seifu ni mkuu katika siasa hata Baba yenu wa Taifa Nyerere akilijua hilo.

  Seif ni mtu ambae anaamsha hisia za wahudhuriaji ,anakipaji hicho cha kuzungumza na kusikika ndani ya mioyo ya waliohudhuria na huwa ni somo tosha, halafu sio nasema hivi kwa kuwa ionekane ndio pekee ,hapana Slaa,Mbowe nafikiri Zitto hawa wote natumai wamewahi kupewa muda wa kuzungumza katika mikutano ya CUF-Zenji hivyo ni utamaduni ambao unaweza kuendelezwa aidha kwa kukusanya wananchi kuna wengine wakisikia Seif leo atatingisha mkutano basi wao watafanya kila kitu ili kuhudhuria na ndio hivyo hivyo hawa akina Slaa huwa wanaalikwa kwenye mikutano ili kuvutia wananchi na ndivyo wapinzani wanavyotakiwa wafanye ili kutoa uzito kwa wananchi waweze kuhudhuria,
   
 20. T

  TanzActive JF-Expert Member

  #20
  May 1, 2009
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 350
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Mbona Slaa is better than Kikwete ,Mkapa and Mwinyi ,the only problem for him to get to Ikulu ni mwamko mdogo na uelewa mdogo wa wapiga kura hasa wa vijijini !!!
   
Loading...